https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    KOCHA WA GOR MAHIA AGEUKA MBOGO KUHUSU OLUNGA

    Olunga 1Kocha mkuu wa timu ya Gor Mahia ya Kenya Frank Nuttal  amegeuka mbogo kwa waandishi wa habari wanaotaka kufanya mahojiano na mchezaji wake Michael Olunga ambaye amejizolea umarufu mkubwa baada ya kuonesha kiwango cha juu kwenye mechi tatu ambazo amecheza huku akifanikiwa kufunga magoli matatu mpaka sasa.
    Waandishi wengi wamekuwa wakitaka kufanya mahojiano na mchezaji huyo hasa baada ya kuhusishwa kutakiwa na vilabu inavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara.
    Olunga mazoeziniBaada ya mazoezi ya jana, mtandao huu ulimfuata Olunga kwa ajili ya kufanya nae mahojiano lakini mchezaji huyo akauambia mtandao huu kuwa, inabidi upate ruhusa kutoka kwa kocha wa timu lakini yeye yuko tayari kuzungumza.
    Mtandao huu ikabidi umvae kocha wa timu hiyo, Nuttal ili upate ruhusa ya kuzungumza na mchezaji huyo lakini kocha huyo akaweka ngumu na kusisitiza hataki mchezaji wake azungumze na vyombo vya habari anahitaji muda wa kutulia.
    Olunga 4Awali mtandao huu ulitafuta nafasi ya kuzungumza na Olunga baada ya mchezo wao dhidi ya KMKM lakini kocha wa timu hiyo alizuia akidai mchezaji wake amechoka anahitaji muda wa kutosha kupumzika.
    Olunga 3Olunga amekuwa akizungumzwa sana kwenye vyombo vya habari tangu kuanza kwa michuano ya Kagame na klabu ya Simba na Azam zinahusishwa kumfukuzia mshambuliaji huyo ambae anakipiga pia kwenye timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA WA GOR MAHIA AGEUKA MBOGO KUHUSU OLUNGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top