ASASI ya kiraia ya Kufuatilia Mwenendo wa
Bunge imesema kwa miaka mitano sasa, kiti cha Spika wa Bunge la
Tanzania Anna Makinda kinatumia kanuni vibaya kwa lengo la kukumbatia
ufisadi kwa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Kauli hiyo inakuja baada ya Makinda,
Bunge kuwafukuza bungeni wabunge 46 kati ya wabunge 90 wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni mwishoni mwa wiki.
Fukuza fukuza hiyo ilifanyika baada ya wabunge hao kupinga kupitishwa kwa hati ya dharura : Muswada wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015; Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015; Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Katika Tasnia ya Uchimbaji Tanzania wa Mwaka 2015.
Akizungumza na MwanaHALISI Online Albanie
Marcossy, Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo amesema, “…hakuna shaka
kufukuzwa kwa wabunge wa upinzani ni mwendelezo wa udhaifu wa kiti cha
spika kwa miaka mitano tangu mwaka 2010.”
“Lengo ni kulinda ufisadi na mambo
yanayopagwa kinyume na maslahi ya umma. Imeleta hasara kubwa. Maamuzi
mengi yanapita kwa maslahi ya wachache,” amesema Marcossy.
Sakata la wabunge kupiga miswada hiyo,
lilianza Juni 29 mwaka huu wakati wabunge wote walipokutana na wadau wa
sekta ya nishati kujadili miswada hiyo mjini hapa.
Wakati wa semina hiyo, wabunge wa
upinzani na CCM waliungana kuipinga miswada hiyo ambapo Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Charles Mwijage, alimrushia maneno ya kashfa Mbunge
wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM) baada ya mbunge huyo kuikataa miswada
hiyo.
credit: mwanahilisi online
0 comments:
Post a Comment