Waziri Mkuu wa zamani na aliyekuwa mtangaza nia ya kugombea urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu zilizosainiwa na wadhamini wake.
TAYARI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Waziri wa Ujenzi, John Pombe Joseph Magufuli kuwa mgombea urais mwaka huu huku Samia Suluhu Hassan akiwa mgombea mwenza, lakini bado jina la mgombea aliyekatwa, Edward Lowassa linazungumzika, safari hii yakibainishwa mambo matano yanayoolezwa ndiyo yalichangia kukatwa kwake.
Akizungumza na Uwazi juzi mjini hapa kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya CCM-Taifa (Nec) alisema nguvu ya Lowasaa kichama ilikuwa kubwa lakini mambo hayo matano ndiyo yalisababisha akashindwa kufikia hata hatua ya Tano Bora.
“Sisi kama wajumbe, tunajua mengi. Lowassa alikuwa mgombea mwenye nguvu, alikuwa na watu ndani ya Nec, lakini sasa Kamati Kuu (CC) ilimkata kwa vigezo vyake, lakini naamini ndani ya hayo mambo matano ndiyo maana alikatwa.
MAKANISA, MISIKITI YATAJWA
Kwa mujibu wa mjumbe huyo kutoka Mkoa wa Tanga, kitendo cha Lowassa kuchagisha fedha kwa njia ya harambee kwenye misikiti na makanisa akiwa kama mgeni mwalikwa, kulichangia CC ya CCM kumwona kama alianza kampeni mapema.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo kutoka Mkoa wa Tanga, kitendo cha Lowassa kuchagisha fedha kwa njia ya harambee kwenye misikiti na makanisa akiwa kama mgeni mwalikwa, kulichangia CC ya CCM kumwona kama alianza kampeni mapema.
“Unajua ndani ya makanisa mengi yanasemwa. Baadhi ya watu ndani ya chama chake walisema alianza kampeni mapema kwa vile kule kuzungumza na waumini kuliweza kumpa nguvu ya kisiasa. Hii nayo ilichangia,” alisema mjumbe huyo.


0 comments:
Post a Comment