Ralph R. Debbas, ni mkurugenzi wa kampuni mpya ya magari W Motors iliyopo Dubai. Na baada ya ujio wao kwenye ulimwengu wa magari, kampuni hii imeanza kutengeneza headlines za kipeke duniani, ikiwa ni kampuni ya kwanza ya kiarabu kutengeneza magari yanayoipiku brand kubwa za magari duniani kama Ferrari, Lambroghini na Buggati.
Mwezi wa sita mwaka huu, Lykan Hypersport lilitangazwa kuwa gari la kwanza la kifahari kutumika na polisi wa Abu Dhabi
W Motors sasa hivi wako mezani na project nyingine ya gari hii itakayoitwa SuperSport Car, yatakayo tengenezwa 25 tu kwa mwaka.
Kampuni hiyo inadhamiria kutengeneza matoleo ya magari yatakayo shindana kwenye soko na matoleo ya Ferrari, Lamborghini na Bugatti.
Gari hili likikamilika litauzwa kuanzia dola 250,000 na litakuwa linatengenezwa Dubai tu kwenye kiwanda hicho kipya.


0 comments:
Post a Comment