Michezo ya robo fainali itaanza kupigwa siku ya Jumanne tarehe 28 Julai ambapo mchezo wa kwanza utakaoanza saa 8:00 mchana utakuwa ni kati ya Al Shandy ya Sudan dhidi ya KCCA ya Uganda wakati mchezo wa pili utawakutanisha timu wenyeji wa mashindano Yanga dhidi ya Azam FC mechi itakayoanza saa 10:00 jioni mechi zote zikipigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Michezo mingine ya robofainali itaendelea siku ya Jumatano tarehe 29 Julai wakati wababe wa Kenya timu ya Gor Mahia itakapo pambana na Malakia FC ya Sudan Kusindi huku APR FC ya Rwanda ikichuana na Khartoum National Club ya Sudan.
Kutokana na ratiba hiyo, inamaanisha timu moja ya Tanzania kati ya Azam FC au Yanga lazima iyape mkono wa kwaheri mashindano hayo na kuipisha timu moja isonge mbele kwenye hatua ya nusu fainali.
Hii hapa ratiba kamili ya michezo ya robo fainali;
Al Shandy (Sudan) vs KCCA (Uganda)
Azam FC (Tanzania) vs Yanga (Tanzania)
Gor Mahia (Kenya) vs Malakia FC (Sudan Kusini)
APR FC (Rwanda) vs Khartoum National Club (Sudan)
0 comments:
Post a Comment