Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea ushindi wao wa Ngao ya Jamii leo baada ya kuifunga Chelsea 1-0 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA
Mfaransa Arsene Wenger amevunja ‘uteja’ wake kwa Mreno, Jose Mourinho
leo. Wenger ameshinda mechi ya kwanza dhidi ya Mourinho katika mechi 14,
baada ya kuiwezesha Arsenal kutwaa Ngao ya Jamii England kwa ushindi wa
1-0 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Wembley, London.
Hilo
ni taji la pili ndani ya miezi mitatu kwa Arsenal, baada ya miezi
miwili na ushei iliyopita kutwaa Kombe la FA katika fainali iliyopigwa
uwanja huo huo.
Kipa
wa zamani wa Chelsea, Petr Cech alidaka kwa ustadi mkubwa huku bao
pekee la Arsenal likifungwa na kiungo Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya
24.
Kikosi
cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal,
Coquelin, Ramsey, Oxlade-Chamberlain/Arteta dk77, Cazorla, Ozil/Gibbs
dk82 na Walcott/Giroud dk66.
Chelsea:
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry/Moses dk82, Azpilicueta/Zouma dk69,
Matic, Ramires/Oscar dk54, Willian, Fabregas, Hazard na Remy/Falcao
dk45.
0 comments:
Post a Comment