Katika hali ya kuendelea
kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya mchakamchaka wa ligi kuu msimu ujao
timu ya Simba SC leo imeshusha kifaa kingine kutoka Zimbabwe akiwa ni
kiungo mshambuliaji Justice Majabvi ambae tayari ameanza mazoezi na
kikosi cha msimbazi kilichopiga kambi yake visiwani Zanzibar kwa ajili
ya kufanya mazoezi kujiweka tayari na msimu ujao wa ligi.
Kiongozi wa kambi ya Simba
visiwani Zanzibar Abuli Mshangama amesema tayari mchezaji huyo ametua
Zanzibar akitokea Vietnam lakini hajasema mchezaji huyo wamemsajili kwa
mkataba wa miaka mingapi.
Katika hatua nyingine, ‘Wekundu
wa Msimbazi’ jana usiku walitoa kipigo kingine visiwani Zanzibar ambapo
waliilaza timu ya Polisi kwa goli 2-0 kwenye pambano lililofanyika
kwenye uwanja wa Amaan.
Magoli ya Simba yamefungwa na
Elias Maguri pamoja na Mussa Hassan ‘Mgosi’, Simba itaendelea na ratiba
ya kucheza mechi zake za kirafiki ikwa visiwani Zanzibar ambapo
Jumatatu itakutana na Jang’ombe Boys na mechi yao ya mwisho ya kirafiki
itachezwa dhidi ya KMKM ambayo imetoka kwenye michuano ya Kagame siku
chache zilizopita
0 comments:
Post a Comment