Mtendaji mkuu wa Azam Media Limited Rhys Torrington akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa channel mpya ya michezo
Mtendaji mkuu wa Azam Media
Limited Rhys Torrington amesema lengo la kuanzisha channel hiyo ni
kuhakikisha watazamaji wa Azam TV hasa wapenda michezo wanapata fursa ya
kutazama ligi kuu ya Hispania pamoja na VPL lakini bila kusahau michezo
mingine ukiondoa soka.
Torringson ameongeza kuwa, mbali
na kupata fursa ya kuangalia michezo kwenye channel inayojitegemea,
watazamaji wataona picha ambazo ni ang’avu (HD) na zenye ubora wa hali
ya juu kupitia channel hiyo.
Vijana wakionesha baadhi ya jezi ambazo huvaliwa na timu zitakazokuwa zinaonekana kupitia Azam Sports HD
Kwa upande wa naibu mtendaji mkuu
wa Azam Media Limited Bw. Tido Mhando yeye amesema mbali na watazamaji
kutazama picha ang’avu, watapata fursa ya kupata uchambuzi na matangazo
ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiswaili kutoka wa watangazaji wa michezo
wa kituo hicho.
Mtangazaji mkongwe wa Tanzania
ambaye alikuwa akitangaza kwa Kiswahili kwenye Shirika la Utangazaji
nchini Uingereza Charles Hilary amesema yeye pamoja na timu yake nzima
ya watangazaji wa habari za michezo wa kituo hicho wamejipanga
kuhakikisha watazamaji wanapata burudani kupitia channel hiyo mpya ya
michezo.
Hilary akiwa ndiye kiongoi wa
timu ya watangazaji wa michezo pamoja na wachambuzi, amekitaja kikosi
anachokiongoza kinachoundwa na watangazaji na wachambuzi wafuatao;
Watangazaji
1. Charles Hilary
2. Baruani Mhuza
3. Patrick Nyembelan
4. Philipo Cyprian
5. Twalib Omary
6. Ahmed Abdallah
7. Rehema Jarufu
8. Shezia Mugilwa
9. Michael Malue
Wachambuzi
1. Eddo Kumwembe
2. Ally Mayay
3. Jeff Lea
4. Karly Ongala
5. Hussein Sappi


0 comments:
Post a Comment