NYOTA
Aritz Aduriz amepiga mabao matatu peke yake, Athletico Bilbao
ikiiandika Bacelona 4-0 katika mchezo wa Super Cup ya Hispania usiku huu
Uwanja wa San Mames Barria.
Mikel
San Jose alianza kumtungua kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen
dakika ya 13 kabla ya Aduriz kufunga mabao mawili ya haraka haraka
dakika za 53 na 62.
Aduriz
akakamilisha hat-trick yake kwa bao la mkwaju wa penalti, baada ya beki
Dani Alves kumchezea rafu. Lionel Messi na Luis Suarez wote walikuwapo
katika safu ya ushambuliaji ya Barca, lakini wa Bilbao ulikuwa mzito
kwao kuuangusha.
Kikosi
cha Athletic Bilbao kilikjwa; Iraizoz, Laporte, San Jose, Balenziaga,
Etzeita, Benat, Susaeta/Boveda dk85, Eraso/Gurpegi dk77, De Marcos,
Sabin/Lekue dk66 na Aduriz.
Barcelona;
Ter Stegen, Alves, Vermaelen, Bartra, Adriano, Mascherano,
Rafinha/Iniesta dk52, Sergi Roberto/Rakitic dk60, Messi, Suarez na
Pedro/Sandro dk71.
Tegemeo la Barcelona, Lionel Messi akiwa taaban baada ya kipigo cha Athletic Bilbao PICHA ZAIDI GONGA HAPA



0 comments:
Post a Comment