https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    CHELSEA HOI KWA MAN CITY, YAKUBALI KIPIGO BAO 3


    Sergio Aguero akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa klabu yake.
    Magoli ya Sergio Aguero, Vincent Kompany na Fernandinho yamepeleka kilio kwa Chelsea dhidi ya Man City katika ushindi wa mabao 3-0, mchezo uliopigwa katika dimba la Etihad.
    Chelsea ambao leo walionekana kutepeta hasa katika eneo la kiungo wamekosa tena alama tatu muhimu mara baada ya mchezo wa awali kulazimishwa sare na Swansea katika uwanja wao wa nyumbani.
    Dhamna kubwa ilikuwa kwa upande wa Ivanovic ambaye siku ya leo ama hakika atalala na viatu mara baada ya kusumbuliwa vilivyo na winga mpya wa Man City aliyesajiliwa kutoka klabu ya Liverpool Raheem Sterling ambaye kwa siku ya leo alikuwa chachu kubwa ya ushindi wa Man City.
    Kwa upande wa Diego Costa leo alibanwa vilivyo na mabeki visiki wa Man City Eliaquim Mangala pamoja na Vincent Kompany
    Vikosi vilikuwa hivi:
    MANCHESTER CITY: Manchester City: Hart, Sagna, Mangala, Kompany, Kolarov, Toure, Fernandinho, Navas (Nasri 65mins), Silva, Sterling (Demichelis 79), Aguero (Bony 83)
    Benchi: Caballero, Zabaleta, Clichy, Iheanacho
    Waliopewa kadi: Kompany, Fernandinho, Mangala, Toure
    Goal: Aguero 34, Kompany 79, Fernandinho 85 
    CHELSEA (4-2-3-1): Begovic, Ivanovic, Cahill, Terry (Zouma 45), Azpilicueta, Ramires (Cuadrado 64), Matic, Willian (Falcao 79), Fabregas, Hazard, Diego Costa
    Benchi: Blackman, Mikel, Loftus-Cheek, Remy  
    Waliopewa kadi: Ivanovic, Hazard
    Refarii: Martin Atkinson
     Vincent Kompany akishangilia goli.
    Fernandinho akishangilia mara baada ya kufunga bao la tatu kwa Man City
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA HOI KWA MAN CITY, YAKUBALI KIPIGO BAO 3 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top