Defensive, Deep-Lying, Central, Attacking Midfielders hawa ni baadhi ya viungo wachache kati ya wengi ambao wanahitaji ubunifu na nguvu za kutosha. Achana na Offensive Midfielders ila hao hapo juu mara nyingi wameonekana wanaamua timu icheze vipi. Claudio Makele baada ya kuondoka Real Madrid ilichukua muda mrefu sana Madrid kurejea kwenye kiwango, pia hata kabla ya ujio wa Nemanja Matic pale Chelsea, akina Essien, Ballack na Mikel Obi walijaribu kuziba pengo la Makele pale Chelsea lakini hawakufanya kwa 100%. Kutokana na nafasi ya kiungo kuwa muhimu leo naomba tuwe pamoja hadi mwisho…
Leo naomba tuwatazame viungo ambayo wameacha mashimo makubwa tangu waondoke kwenye vilabu vyao, mashimo ambayo bado hayajafukiwa hadi leo na kusababisha vilabu hivi kuyumba katika sehemu ya katikati na hata kukosa ubunifu kama ule wa viungo hawa waliokwenda kutafuta maisha
katika timu zingine, karibu…
XABI ALONSO-LIVERPOOL
Tangu anatua Liverpool mwaka 2004 akiwa sambamba na Luis Garcia chini ya Benitez, Xabi alonso aliendelea kuwa kiungo muhimu sana sehemu ya kiungo cha Liverpool, ukweli ni kwamba kiwango cha Gerald kilikuwa kikubwa sana kipindi hiki kutokana na kucheza sambamba na fundi Alonso, pasi zake za umbali mrefu zilisaidia sana washambuliaji na viungo wa Liverpool. Kwa watu wanaofatilia mpira wataungana na mimi kuwa ‘Perfomance’ ya Gerald na Liverpool viliporomoka sana tangu 2009 Alonso alipoondoka Anfield. licha ya Liverpool kumsajili Alberto Aquilani kumrithi Alonso, bado ilizidi kufanya vibaya sehemu ya kati.
Na hata kufikia kukosa michuano ya Uefa mara 5 mfululizo, majeraha yalimsumbua Aquilan na kuwapa mwanya viungo wengine kama Raul Meireles, Charlie Adam, Christian Poulsen na Jonjo Shelvey kuja
kujaribu kuziba pengo hili. Kuja kwa hawa hakukufanya pengo la Alonso kuzibika na hata kufikia hatua ya Lucas Leiva kusajiliwa lakini bado hakuziba pengo la Alonso. Ni miaka 6 sasa bado hajatokea kiungo
anayekaba, kushambulia, kupiga pasi fupi na ndefu, kupooza mashambulizi na ku-balance timu muda wote wa mchezo. pengo hili pia linawagharimu Real Madrid kwa sasa.
LUCA MODRIC-TOTTENHAM HOTSPURS
Dinamo Zagreb ilimuuza kiungo Luca Modrid kwenda Tottenham mwaka 2008. Usajili huu unaweza kuwa bora kwa Spurs na utakumbukwa sana kwani ndani ya muda mfupi Modric alipata umaarufu mkubwa kutokana na kiwango chake. Tangu asajiliwe Spurs, timu yake ili Improve sana hadi kufikia
hatua ya kuwa miongoni mwa timu za Top 4 kwenye msimamo wa Epl na hata kushiriki Uefa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, Real Madrid walimwaga pesa za kutosha pale White hart lane na mwaka 2012 aliwaaga mashabiki wa Spurs pale London. Tottenham walijifariji kwa kuwasajili viungo kama Holtby, Capoue, Paulinho na Stambo
Lengo lilikuwa kuimarisha safu ya kiungo cha kati lakini wachezaji hawa walishia kufanya vibaya hata kukosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza. Mousa Dembele alisajiliwa kuziba pengo la Modric ila hadi sasa anashindwa ku-control mechi kama alivyokuwa anafanya Modric na hii ni sababu Spurs hadi sasa inakosa ubunifu kama ule wa Modric wa kuwafungua wapinzani na kuwapa mwanya washambuliaji kufanya yao. Mpaka sasa Madrid wanafurahia ubunifu wa Modric na hawatamani kusikia dili lolote kutoka sehemu yoyote kumng’oa kiungo huyu.
PAUL SCHOLES-MANCHESTER UNITED
Bila shaka ukimuuliza mshabiki yeyote wa Man U akutajie viungo wawili waliofiti pale katikati kwa kipindi cha miaka 15 ya karibuni asipokutajia Carick na Paul Scholes basi huyo sio shabiki wa kweli.
Paul Scholes hadi sasa mbadala wa nafasi yake hajapatika pale Old Traffordt, licha ya kustaafu msimu wa 2010/11 ilimchukua miezi 6 pekee kubadilisha maamuzi yake ya kustaafu baada ya mapungufu makubwa kujitokeza kwenye safu ya kiungo cha Man U. Baada ya kustaafu moja kwa moja matumaini ya mashabiki wa united yaliamia kwa akina Tom Cleverley na Anderson, ila walishindwa kufanya yale aliyokuwa anayafanya Scholes dimbani.
Tangu aondoke hadi leo anakosekana kiungo ambaye anaweza kubadilisha mwelekeo wa mechi, kiungo anaye-balance timu na anayewasoma wapinzani na kufanya maamuzi panapostaili. United kwa sasa ina viungo wazuri ila bado hawajafikia hata nusu ya kiwango cha Scholes kitu ambacho kinawafanya washambuliaji ni viungo wengine kukaba sana kwa ushirikiano ili timu ifanye vizuri, bila shaka mbinu mpya za Van Gaal ndizo zinafanya shimo la Scholes lisionekane kwa macho.
ANDREA PIRLO-AC MILAN
Baada ya kukataa kumuongezea mkataba Andrea Pirlo mwaka 2011, hatimaye Ac Milan ilimpoteza kiungo huyu ambaye kipindi hicho alikuwa na miaka 32. Milan walisingizia kigezo cha umri ila Juventus walimchukua bure na kumpa namba kikosini. Akiwa Juve, Pirlo kama kiungo mbunifu aliwasaidia Turin kuchukua vikombe 7 na kufika fainali ya Uefa. Kwa upande wa Milan licha ya kuwasajili akina Muntari, Aquilani, Nocerino, Emanuelson, Flamini, Essien na Poli waliishia kuteseka na hata kumaliza ligi wakiwa nafasi ya 10, 8 na walijatahidi sana misimu miwili kumaliza nafasi 2 na ya 3…
Montolivo aliaminiwa na mashabiki wa Milan kuwa ataweza kurithi nafasi ya Pirlo ila mambo yalizidi kwenda kombo pale Ac Milan na kuzidi kutimua Makocha kwa kuzani wanachangia matokeo mabovu, kumbe ni timu kushindwa kusajili wabunifu kama akina Pirlo na mwenzake Kaka. Pirlo ili kuwaonesha kuwa yeye ni mwiba, alichukua tuzo za mchezaji bora wa ‘Serie A’ mara 3 mfululizo tangu 2012 hadi 2014. Bila shaka hata kuondoka kwake pale Juve kutaacha pengo kubwa sana msimu huu kwani
hata Vidal pia ameondoka.
PATRICK VIERA-ARSENAL
Japokuwa ni muda mrefu tangu Defensive Midfielder bora wa muda wote pale Arsenal, Patrick Viera astaafu, hakuna kiungo mwingine aliyekuja London na kukaa muda mrefu kwa mafanikio pale Arsenal. Abou Diaby alitajwa sana kuchukua nafasi yake ila majeraha yalionekana kumkwamisha Mfaransa huyu. Mbali na huyu pia Alex Song na Denilson walijaribu bila mafanikio na tumaini la mwisho lilikuwa ni Jack
Wilshere ambaye majeruhi yamekuwa yakimuandama kila siku. Baada ya Wenger kushindwa kumpata kiungo kama Viera, alimbadilishia majukumu Mikel Arteta kucheza kama ‘Deep-lying midfielder’
Majukumu haya hayatofautiani sana na yale ya Viera, ila bado vijana hawa wameshindwa kuwa na nguvu na juhudi kama zile za Viera… hali hii ilisababisha kuja kwa Francis Coquelin ambaye kwa mbaali anafata nyayo za Viera ila bado anakosa ubunifu wa kupiga zile ‘tacke’ na kuzuia mashambulizi ya wapinzani kwa wakati, kama atapewa muda huenda akaziba shimo hili lilioachwa na Mfaransa huyu.


0 comments:
Post a Comment