Manchester city wameonekana kuwa na kikosi kizuri sana kwenye mechi za ufunguzi wa EPL baada ya kuichapa Chelsea 3 bila majibu. Lakini bado hawajalidhika na usajili huo bado wanaendelea kusajili wengine.
Ripoti mpya hivi sasa ni kwamba Man city wametoa kiasi cha £50 million kwa ajili ya kumsajili midfielder wa Wolfsburg Kevin De Bruyne. Mchezaji huyu mwenye miaka 24 anategemewa kuja kuongeza nguvu kwenye harakati za kunyakua taji la EPL, akiwa Wolfsburg ameweza kufunga magoli 10 na kutoa assist 20 zilizozaa magoli.
Dili hili linategemewa kukamilishwa kwenye siku chache zijazo na kuungana na kikosi cha Manchester city


0 comments:
Post a Comment