KLABU
ya Manchester City imetangaza kumsajili kiungo wa zamani wa Chelsea,
Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg ya Ujerumani kwa dau la Pauni Milioni
52.
Mbelgiji
huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alicheza kwa miaka miwili Stamford
Bridge kabla ya kuhamia Bundesliga mwaka 2014, alifuzu vipimo vya afya
jana kuelekea uhamisho huo wa dau kubwa.
De Bruyne anaingia kwenye orodha ya wachezaji wengine wapya Man City akina Raheem Sterling, Nicolas Otamendi na Fabian Delph.
Kevin De Bruyne akiwa ameshika jezi ya Manchester City baada ya kukamilisha uhamisho wake Wolfsburg PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment