Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa mkoani simiyu,Adili Elinipenda amsema kuwa dereva
huyo ambaye pia ni mratibu elimu kata ya nyangokolwa wilayani Bariadi,
alikamatwa majira ya saa tano usiku katika kijiji cha nguliguli wilayani
maswa akiwa anaendesha gari hilo ambalo baada ya kulikagua walikuta
pesa kiasi cha shilingi laki nne zenye noti mpya za elfu mbilimbili.
Amesema kuwa baada ya maafisa hao kumhoji amekiri kuwa gari hilo
lilikodiwa kugawa pesa hizo kwa wajumbe na mwenyekiti wa CCM wa wilaya
ya Maswa Peter Bunyogori ambaye pi ni mgombe wa ubunge kwa tiketi ya
chama cha mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment