https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Viongozi wa UKAWA walalamikia uonevu, ukiukwaji wa haki ya kutumia viwanja kufanya kampeni

    .
    Uzinduzi rasmi wa kampeni za uchaguzi wa vyama vinavyounda (UKAWA) huenda ukakwama baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa tareheya uzinduzi huo, uwanja wa Jangwani uliokuwa umepangwa  kutumika utakuwa na kazi nyingine.
    Hata hivyo wakizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mmoja wa viongozi wa umoja huo, Bw James Mbatia wamewataka wananchi wanaotaka madiliko kutokatishwa tamaa na changamoto hizo kwani zinafanywa kwa lengo la kujaribu kudhoofisha vuguvugu la mabadiliko jambo ambalo licha ya kuwa halitafanikiwa.
     
    Aidha Mh Mbatia pia akalalamikia ukiukwaji wa taratibu za kufanya kampeni ukiwemo wa kutumia lugha zinazochochea chuki  na zinazoweza kuligawa taifa.
    Kwa nyakati  tofauti, baadhi ya viongozi wa idara zinazolalamikiwa akiwemo Bw, Paul Chagonja kutoka jeshi la polisi na jaji mkwawa kutoka tume ya uchaguzi wameeleza baadhi ya malalamiko na pia wameendelea kusisitiza suala zima la kila chama na kila mtanzania kuendelea kuheshimu sheria na taratibu.
     
    Kuhusu hofu iliyoanza kujengeka ya kutumia wizi wa kura unaodaiwa kufanywa wakati wa uchaguzi Mh Jaji Mkuwawa amesema sheria ziko wazi na zikifuatwa suala la kuibiwa kura halitakuwepo.
     
    Akizungumza kwa njia ya simu kuhusu malalamiko ya UKAWA kuzuiliwa kutumia uwanja wa Jangwani mkurugenzi wa manispaa ya Ilala amesema hana taarifa rasmi za mabadiliko ya matumizi ya uwanja huo.
     
    Pamoja na heka heka hizo zinazoendelea mh Mbatia amesema wanaendelea kutumia busara na kuhakikisha kuwa uzinduzi wa kampeni zao unafanyika kama ulivyopangwa na amewataka wananchi kuendelea kuwa wapole ili lengo lao la kufanya mabadiliko liweze kutimia kwa  amani kwani UKAWA inamuhitaji kila mmoja
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Viongozi wa UKAWA walalamikia uonevu, ukiukwaji wa haki ya kutumia viwanja kufanya kampeni Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top