WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Misugusugu, wilayani Kibaha mkoani Pwani wamefunga barabara ya Morogoro kufuatia wenzao wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi mapema leo.
Mmoja kati ya wanafunzi hao amefariki dunia huku mwingine akijeruhiwa.
Wanafunzi hao wamegongwa walipokuwa wakitaka kuvuka barabara kuelekea shuleni kwao.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jafari Ibrahimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa mwanafunzi aliyefariki ni wa darasa la tatu na aliyejeruhiwa ni wa darasa la nne.
Kamanda Ibrahimu ameongeza kuwa, dereva wa gari hilo ambaye ni askari amekamatwa na kuwekwa mahabusu kwa uchunguzi zaidi na chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
SOURCE: Globalpublishers
0 comments:
Post a Comment