Watu 220 waliokuwa
wakishiriki sherehe za hija wamefariki kwenye mkanyagano uliotokea
katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca, maafisa nchini Saudi Arabia
wamesema.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema kupitia
Twitter kwamba watu wengine 450 wamejeruhiwa katika kisa hicho
kilichotokea mji wa Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca.Shughuli za uokoaji zinaendelea, idara hiyo imeongeza.
Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya sherehe za Eid al-Adh
CREDIT: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment