https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Hadi kufikia June 2013 haya ndio yalikuwa maajabu 10 ya Dubai (+Pichaz)

    Miongoni mwa sehemu nzuri na zakuvutia kutembelea katika hii Dunia basi Dubai haiwezi kukosa, Dubai unatajwa kuwa mji wa kitalii na kibiashara, wengine wanautaja kama pepo ya watalii. Mji huo umejengeka kwa majengo yenye ramani za kuvutia. September 17 nakusogezea list ya maajabu 15 ya Dubai stori kutoka worldtoptop.com.
    Hadi kufikia June 2013 hizi ni sehemu 10 zilizokuwa zinatajwa kuwa nzuri na zakuvutia Dubai.
    1. Burj al Arab

    Burj_al_arab
    Burj al Arab ni hoteli yenye hadhi ya nyota 7 ina vingi vya kuvutia, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwanja wa tennis ulio juu, mgahawa chini ya bahari. Lakini Burj al Arab ni moja kati ya hoteli zinazoitambulisha Dubai.
    2-Visiwa vya Palm
    Jumeirah_palm_island_dubai
    Visiwa vya Palm ni visiwa vikubwa zaidi vilivyotengenezwa na binadamu sio visiwa vya asili kama ilivyo kwa Zanzibar na vingine, visiwa hivyo vinatajwa kuwa miongoni mwa maajabu 8 ya Dunia.
    3. Burj Khalifa
    Burj-khalifa
    Burj Khalifa inatajwa kuwa jengo refu Duniani lililojengwa na binadamu, Burj Khalifa ni jengo lenye ghorofa 160.
    4. Dubai Marina
    dubai_marina
    Dubai Marina ni mfereji mkubwa zaidi Duniani uliyo jengwa na binadamu, Dubai Marina una sehemu za kupaki boti ndogo lakini ni mji ambao umetengenezwa kuweza kuchukua watu 120000.
    5. Infinity Tower
    infinity_tower_dubai_2
    Infinity Tower ni jengo refu lililo jengwa katika mfumo wa nyuzi 90 na lina urefu wa futi 1000 kutoka chini.
    6- Dubai Mall
    dubai_mall_1 (1)
    Dubai mall ni mall yenye eneo kubwa duniani na ina hifadhi ya wanyama ya kutengeneza, ina vyumba 250 vya Luxury hoteli lakini ina chem chem.
    7. Jumeirah Beach Hotel
    jumeirah_beach_wave_hotel
    Jumeirah Beach Hoteli ni hoteli yenye hadhi ya nyota 5 , ramani yake ni kama wimbi la maji ya bahari.
    8. Dubai Fountain
    Dubai_fountain
    Hii ni chem chem iliyopo Dubai kama hufahamu chem chem ni maji yatokayo ardhini lakini yanatoka yakiwa na presha.
    9.  Atlantis The Palm Hotel & Resort
    atlantis_hotel_dubai_1
    Atlantis The Palm Hoteli & Resort ni hoteli yenye vyumba vya kulala chini ya maji ambapo ukilala katika hivyo vyumba unaweza pata nafasi ya kuona samaki wakubwa kama papa na wengineo.
    10. Ski Dubai
    Ski-dubai
    Ski Dubai ni sehemu yenye theluji ina ukubwa wa mita za mraba 22500, inatumika kama sehemu ya kuenjoy kwa baadhi ya michezo ambayo huchezwa sehemu kama hizo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hadi kufikia June 2013 haya ndio yalikuwa maajabu 10 ya Dubai (+Pichaz) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top