https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    HIZI NI MECHI 10 ZILIZOWA DISAPPOINT SANA MASHABIKI WA ARSENAL KWENYE UEFA…YA JANA IPO NAMBA NGAPI?

    arsenal
    Kama wewe ni shabiki wa Arsenal na umekua dissapointed kwenye mechi ya jana basi kuna wenzako walioshudia hizi mechi kumi pia walikua na hali kama yako. Hizi hapa ni mechi 10 ambazo perfomance mbovu ya club ya Arsenal kwenye UEFA. Soma na unipe maoni yako kwenye hii list.
    10. Arsenal 0-1 Lens November 1998
    Mwaka huu kwenye Arsenal waliishia njiani kwenye harakati zao za kuelekea kwenye fainali ya UEFA baada ya kufungwa na RC Lens. Kwenye mechi ya kwanz walifungwa na Dynamo Kiev na baada ya hapo wakachapwa kimoja kwenye uwanja wao nyumbani na RC Lens, Goli la Mickael Debeve lilitupa Arsenal nje ya mbio za UEFA licha ya kushinda game ya mwisho ya kwenye kundi lao.
    9. Arsenal 3-3 Anderlecht November 2014
    Arsenal japokua iliendelea mbele lakini iliwaangusha sana mashabiki wake kwenye hii mechi. Arsenal walikua mbele kwa magoli 3 bila hadi half time. Lakini walivyorudi mambo yaliwageukia na Vanden Borre kutupia mbili na bada Mitrovic kumalizia dakika ya 90.
    8. Arsenal 1-3 Bayern Munich February 2013
    Mechi hii haikua ni aibu kwa Arsenal kufungwa kwasababu kikosi walichokua wanacheza dhidi ya Barcelona ni kikali sana. Lakini kwa ukupwa wa EPL na club kubwa kama Arsenal bila shaka ilitakiwa ku-perform vizuri. Kroos,Mueller na Mandzukic walitupia 3 kwa upande wa Bayern na Podolski kutupia moja.
    7. Arsenal 0-3 Inter September 2003
    Msimu wa 2003-04 ulikua ni msimu mkubwa sana kwa Arsenal ambapo walikua na kikosi kikali sana. Sasa kwenye mechi dhidi ya Inter ambapo kikosi cha inter kilikua ndio kimetoka kwenye fall waifanikiwa kuwafunga Arsenal 3-0. Magoli yakitupiwa na Julio Cruz, Andy van der Meyde,Obafemi Martins.
    6. Arsenal 1-1 PSV March 2007
    Hakuna shabiki wa Arsenal ambae atakua alikasirika baada ya timu yake kufungwa kwenye fainali dhidi ya Barcelona 2006 dhidi ya Barcelona. Lakini kutoka kwenye 16 bora msimu unaofuatia lazima litakua tatizo. Kwenye hii mechi Alex wa Arsenal alijifunga na kuharibu mpango wote.
    5. Arsenal 2-3 Olympiacos September 2015
    Mchezo huu wa jana Arsenal Wenger aliutaja kama Must Win game. Lakini alimchagua kipa wake namba mbili Ospina na kucheza mechi ya nyumbani. Makosa ya mabeki na kipa yakashudia Arsenal ikiruhusu magoli 3 wakiwa nyumbani.
    4. Arsenal 1-3 Monaco February 2015
    Kama kawaida kumilika mpira kwa muda mrefu lakini wakifika mbele ya goli tatizo. Arsenal walichezea goli la kwanza lakini Alex Oxlade-Chamberlain akawarudisha kwenye mchezo tena. Lakini kufumba na kufumbua sekunde 60 walijikuta kuwa nyuma kwa magoli mawili.
    3. AC Milan 4-0 Arsenal 2012
    Kikosi cha AC Milan chenye majina kama Thiago Silva, Marc van Bommell, Clarence Seedorf, Robinho na Zlatan Ibrahimovic kilikua cha hatari sana mbele ya Arsenal. Lakini haijalishi kikosi chochote, Arsenal ni timu kubwa sana kuruhusu magoli 4, watu wengi walitegemea 2-1 au 3-2 kama zikiwa nyingi.
    2. Arsenal 1-3 Manchester United May 2009
    Bora shabiki wa Arsenal afungwe na Barcelona lakini sio Manchester united kutokana na ushabiki wa mchezo. Kikosi cha Manchester kilikua na vipaji kama Wayne Rooney, Cristiano Ronaldo na Carlos Tevez, baada ya dakika ya 11 tu Park na Ronaldo walimaliza ndoto zao. Mambo haya yalifanyika ndani ya uwanja wao wa Emirates na inabaki kuwa nusu fainali ya mwisho kwa Arsenal.
    1. Arsenal 1-2 Chelsea April 2004
    Mwaka huu Arsenal walikua na kikosi kizuri sana ambacho kilikua sio rahisi kupoteza mchezo mbele ya club yoyote ile. Lakini goli la Wayne Bridge liliweka pabaya Arsenal. Kila shabiki ambae aliyeenda kwenye hii mechi alitegemea ushindi kwa kikosi kikali chenye watu kama Pires,Cole,Henry na wengi.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI NI MECHI 10 ZILIZOWA DISAPPOINT SANA MASHABIKI WA ARSENAL KWENYE UEFA…YA JANA IPO NAMBA NGAPI? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top