Na Simon Chimbo
Kumekua na ubishani usio na
mwisho wa kuhusu ipi ni ligi bora barani Ulaya. Kila mmoja amekua
akiongea kufuatana na anachokiamini, lakini hebu leo tuanzie hapa
nilipojaribu kuchambua utofauti wa ligi hizi.
Pamoja na matangazo ya
televisheni kutuambia ligi kuu nchini England Ni bora duniani lakini,
uhalisia unabaki kuwa ligi hiyo inapitia kipindi kigumu hivi sasa.
Kuhangaika kwa vilabu vya
Uingereza katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa misimu miwili hivi
sasa inatuonesha namna gani ligi hiyo inakosa kujiamini na ubora wake
kwa namna nyingine umepungua kiasi.
Utawala wa vilabu vya Bundesliga,
mwaka juzi na sasa Hispania, huku kukikosekana timu ya kutoka England
katika hatua ya robo fainali barani Ulaya inatia shaka ubora wa ligi hii
yenye mashabiki lukuki.
Lakini pamoja na kushuka kwa
ubora wa ligi hii, kuna kitu cha pekee zaidi hakipo katika ligi kuu za
mataifa mengine barani Ulaya, nacho ni ushindani.
Nchini Hispania, ukiacha England
msimu wa 2013-14 pekee ambapo Atletico Madrid walijitutumua na kutwaa
ubingwa lakini bado kuna utawala wa vilabu viwili tu vya Barcelona na
Real Madrid.
Ujerumani, kadhalika tangu
Borrusia Dortmund ianze kuporomoka, imebakia ni ligi ya timu moja tu,
Bayern Munich. Huku pia kukiwa hakuna jipya Ufaransa kwa utawala wa PSG.
PSG ametwaa makombe ya ligi kuu
nchini humo mara tatu mfululizo, na hakuna dalili ya ushindani kutoka
timu nyingine hivi karibuni.
Nchini England, timu tano tofauti
zimetwaa ubingwa kwa kipindi cha miaka 23. Manchester United,
Manchester City, Blackburn Rovers, Chelsea na Arsenal zote zimeonja
ladha ya ubingwa.
Kikubwa hapa England ni jinsi
bingwa anavyopatikana, points nyingi zaidi zinatakiwa kutwaa ubingwa.
Lakini pia ushindani wa timu zinazogombana kubakia kwenye ligi pia ni
kitu kingine tofauti cha kipekee.
Lakini kutokufanya vizuri kwa
timu za England barani Ulaya ni pamoja na ukweli kwamba timu hizi
hazisajili wachezaji wazuri sana ukilinganisha na ligi nyingine.
Chelsea ni mabingwa watetezi wa
ligi nchini England lakini wamemuongeza golikipa Begovic, mshambuliaji
Radamel Falcao na Pedro wakiwa wachezaji pekee wenye majina makubwa. Ni
ngumu kutetea ubingwa ama kuongeza kitu klabu bingwa Ulaya. Wakati
Bayern Munich wamemsajili moja ya viungo bora barani Ulaya Arturo Vidal
na Douglas Costa.
Barcelona mabingwa wa makombe
matatu msimu uliopita wamezidi kujiimarisha kwa kumuongeza Arda Turani.
Wakati huo huo PSG wamemsajili Angel Di Maria.
Kila mtu alishuhudia namna
Manchester United ilivyopotea barani Ulaya baada ya kumuuza Cristiano
Ronaldo na kumpoteza pia Carlos Tevez huku wakiwafidia kwa Antonio
Valencia na Michael Owen.
Hapa ndipo timu za England
zinakwama kwa kiasi kikubwa, Chelsea walikua vizuri wakiwa na kikosi
kizito cha Michael Ballack, Frank Lampard na Makelele katikati ya
uwanja. Leo hii ni ngumu kuwatishia nyau Real Madrid wenye Ronaldo, Bale
na Modric.
Manchester City imeshindwa
kuendelea kuwa sawa tangu kupoteza nyota wake wengi kama Gareth Barry,
Nigel De Jong na sasa wameshindwa kumsajili Paul Pogba, tutegemee nini
klabu bingwa Ulaya.
Tukimalizia na Arsenal, nani
hajui siri ya kilichowafikisha fainali ya klabu bingwa Ulaya 2006? na
kupoteza kwa taabu sana mbele ya Barcelona. Huwezi kumfidia Thierry
Henry na Emanuel Adebayor, ama Mertesacker na Sol Campbell ukaendelea
kuwa sawa.
Mwisho kabisa, huo ndio utofauti
wa ubora wa ligi kuu za barani Ulaya, ingawa mjadala juu ya ipi ni ligi
bora zaidi ni endelevu na hauwezi kuisha pasipo vigezo
0 comments:
Post a Comment