Jeshi la Burkina Faso limefika
katika Jiji la Ouagadougou kushinikiza kujisalimisha kwa kikosi cha
kumlinda rais ambacho kilitangaza mapinduzi siku ya Alhamis.
Mazungumzo baina ya wakuu wa jeshi
pamoja na walinzi wa rais yanaendelea kwa mujibu wa vyanzo
mbalimbali.
Kiongozi wa mapinduzi hayo Jenerali
Gilbert Diendere ameviambia vyombo vya habari yupo tayari kukabidhi
madaraka iwapo mpango wa kumaliza ghasia utaoungwa mkono na viongozi
wa kikanda.
Kiongozi wa mapinduzi Jenerali
Gilbert Diendere
0 comments:
Post a Comment