https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Kumbe Ryan Giggs sio mbadala wa Louis van Gaal!!! huyu ndio anatajwa kuchukua nafasi yake 2017.

    Baada ya kocha wa sasa wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal kusema kuwa mipango yake ya kustaafu soka baada ya miezi 18 ijayo iko pale pale, wengi walianza kujiuliza maswali ni nani klabu ya Manchester United inamuangalia kama mbadala wake?
    Manchester-United-v-Swansea
    Ryan Giggs kushoto na Louis van Gaal
    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu wakati anajiunga na klabu hiyo ya Old Trafford mwaka 2014, maamuzi yake ni yale yale. Wengi walikuwa wanatazamia baada ya kustaafu Louis van Gaal mwaka 2017, atakayekuwa mbadala wake ni Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi wa klabu hiyo.
    pg-68-garside-pa
    Pep Guardiola
    Stori kutoka mirror.co.uk ni kuwa mbadala wa Louis van Gaal baada ya kustaafu anatajwa kuwa sio Ryan Giggs ni kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na klabu ya FC Bayern Munich Pep Guardiola. Van Gaal ambaye ametumia pound milioni 90 kusajili wachezaji makinda kama Anthony Martial, Luke Shaw na Memphis Depay inaripotiwa kuwa mpango wake wa kustaafu soka 2017 uko pale pale.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kumbe Ryan Giggs sio mbadala wa Louis van Gaal!!! huyu ndio anatajwa kuchukua nafasi yake 2017. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top