Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.
PSPF
Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo
refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa
mita 147.Majengo
mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika
Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita
173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria,
Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met
Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.
Jengo
hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake
ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi
bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88.
Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la
kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu
nyingine muhimu.
Kudumu
kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa
mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine
yanayochipua kwa kasi katika Afrika.


0 comments:
Post a Comment