Na Salym Juma
Mambo vipi ndugu yangu unayewekeza muda wako kusoma ukurasa huu? Naamini wewe ni mzima na unasubiri Octoba 25 ukafanye uamuzi sahihi usio wa kishabiki. Mimi pia namshukuru Mungu bado nahema kwani hata juzi nilifanikiwa kumuona Fabregas akimpotezea De Gea kwa kutompa
mkono. Pia rehema za Mungu zimenipa pumzi na hata juzi nilimuona kiongozi fulani akiaibika baada ya kuwataka Wabongo kuingia bure kipindi cha pili kwenye mechi ya Stars. Namshukuru Mungu pia naanza kuziona figisufigisu za uchaguzi ujao wa FIFA.
mkono. Pia rehema za Mungu zimenipa pumzi na hata juzi nilimuona kiongozi fulani akiaibika baada ya kuwataka Wabongo kuingia bure kipindi cha pili kwenye mechi ya Stars. Namshukuru Mungu pia naanza kuziona figisufigisu za uchaguzi ujao wa FIFA.
Inashikilia rekodi ya kuwa timu iliyochezesha wachezaji wote 23 kwenye kombe la dunia lililopigwa Brazil. Ni miongoni mwa timu ambazo ziliwahi kufuzu kwenda kombe la dunia bila kupoteza mechi yoyote.
Ikiwa kwenye nafasi nzuri ya viwango vya FIFA mwaka 2012, ilifungwa mechi zote za Euro kwenye hatua ya makundi. Pia ni miongoni mwa timu chache zilizoshiriki kombe la dunia mara nyingi na kufika mbali bila kunyanyua Kombe hili. Wachezaji wake walipata kadi 9 za njano kwenye fainali ya kombe la dunia dhidi ya Hispania mwaka 2010 pale South Africa.
Kutokana na kufanya madudu kwenye michezo ya kufuzu kwenye fainali za Euro, leo hii nimejaaliwa kukuletea sababu 6 nzito ambazo pengine zinapelekea timu hii kufanya vibaya kipindi hiki.
KUTOCHEZA KWA UMOJA KAMA TIMU
Tangu kuondoka kwa meneja Louis Van Gaal, Wadachi wameshindwa kabisa kucheza kitimu na hili linadhihirishwa na mechi 8 walizocheza karibuni kwani viungo wametengeneza assist 4 pekee huku Nigel de Jong na Jordy Clasie wakishindwa kabisa kusaidia mashambulizi. Viungo washambuliaji kama Wesley Sneijder na Georginio Wijnaldum wameshindwa kabisa kuwafungua mabeki ili washambuliaji wafanye yao. Japokuwa walitawala mechi dhidi ya Iceland ila mawinga kama Mephis Depay, Arjen Roben na Narsingh bado hawakucheza kitimu. Idara zote zinaonekana kukosa umoja ndani ya uwanja.
MAJERUHI KWA BAADHI YA WACHEZAJI
Inawezekana sababu hii ikawa na mashiko sana kwani unapozungumzia mabeki hodari wa Uholanzi huwezi kumuacha Ron Vlaar, Wabrazil wanamkumbuka vyema. Kijana huyu amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara. Robin Van Persie pia ni miongoni mwa wachezaji ambao hawapo katika viwango vyao kisa majeraha ya hivi karibuni. Arjen Roben pia amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara kwani amecheza mechi 4 kati ya 8 za kufuzu. Roben pia hakucheza dakika zote kwenye mechi dhidi ya Iceland. Wachezaji hawa walikuwa nguzo muhimu kwenye timu ya taifa.
SAFU MBOVU YA ULINZI ILIYOKOSA MASHIKO
Inawezekana majeraha ya Ron Vlaar yamechangia safu mbovu inayoruhusu magoli kienyeji bila sababu za msingi. Stefan de Vrij na Bruno Martins bado wanaonekana kukosa mtu wa kuongoza pale nyuma kitu ambacho kinaigharimu timu hii hadi sasa. Daley Blind kama beki wa kushoto bado anashindwa kuonesha yale ambayo siku zote anayafanya pale United. Licha ya kumpa nafasi bwana mdogo Jairo Reidewald kwenye mechi iliyopita bado safu haikutulia kwani dogo alichemsha sana. Wachezaji wote wanne wanaocheza pale nyuma bado wanaandamwa na viwango vibovu na kukosa ushirikiano baina yao
UMRI MKUBWA WA SAFU YA USHAMBULIAJI
Hapa ndio patamu ambapo siku zote huwa nazungumza ila watu wananipuuza. Arjen Roben ana miaka 31, Robin Van Persie 32, Klaas-Jan Huntelaar 32 na Wesley Sneijder 31 hawa wote wanategemewa kuongoza mashambulizi ya Uholanzi. Hivi inakuaje wanapokutana na mabeki vijana
wa Iceland waliocheza ‘U-21’ mwaka 2011? Bila kupepesa macho hawa jamaa wamechoka na ni muda wa kuwapa vijana nafasi ili kutengeneza safu mpya ya ushambuliaji. Kuna vijana wazuri kama Luciano Narsingh na Luuk de Jong ambao ni wazuri kama wakiaminiwa. Bila kufanya hivi hali itazidi kuwa mbaya.
wa Iceland waliocheza ‘U-21’ mwaka 2011? Bila kupepesa macho hawa jamaa wamechoka na ni muda wa kuwapa vijana nafasi ili kutengeneza safu mpya ya ushambuliaji. Kuna vijana wazuri kama Luciano Narsingh na Luuk de Jong ambao ni wazuri kama wakiaminiwa. Bila kufanya hivi hali itazidi kuwa mbaya.
BENCHI LA UFUNDI HALIJATULIA
Tangu kuondoka kwa meneja Van Gaal, Waholanzi naweza kusema kuwa bado hawajampata Kocha mwingine mwenye misingi ya uwajibikaji kama Van Gaal. Guus Hiddink ni Kocha mzuri ila alifanya vibaya sana baada ya kuichukua timu kwa Van Gaal. Nadhani kuna kitu kimejificha chini ya kapeti ndani ya benchi la ufundi la Uholanzi ambacho sisi watu wa kawaida hatukijui. Baada ya vipigo, Hiddink aliondoka na kumpisha Danny Blind. Kocha huyu ameanza vibaya sana na kama asipotulia huenda akapumzika muda sio mrefu hasa kutokana na ukweli kuwa Waholanzi hawatavumilia upuuzi wa kupigwa kila mechi.
MAFANIKIO YA YAMEWALEWESHA
Inawezekana ukaipuuza sababu hii, ila ukweli ni kwamba japokuwa Waholanzi hawajawahi kuchukua ubingwa wa dunia ila tangu 2007 hadi 2014 wameonekana kuimarika na hata kufikia hatua ya kushika nafasi ya kwanza mwaka 2011 kwenye viwango vya FIFA. Walicheza fainali mwaka 2010 pale Johanesburg huku pia wakitolewa nusu fainali kwa mikwaju ya penati na Argentina pale Brazil. Hatua hii ni kubwa sana kwa ngazi ya timu ya taifa kwani wachezaji kibao waliopata mafanikio haya bado wapo kikosini. Wachezaji wote wa timu hii wanapaswa kuandaliwa kisaikolojia muda wote wa mchezo.


0 comments:
Post a Comment