Tevez alimvunja mguu Ham wakati
wawili hao walipokuta wakaiwa wanawania mpira kwenye mchezo wa ligi kuu
ya Argentina (Primera Dicision) ambapo Boca waliibuka na ushindi wa goli
3-0 huku picha za tukio hilo baya zikisambaa duniani kote.
Lakini inaonekana kama mchezaji
huyo wa Argentinos amefurahishwa na Tevez kwenda kumjulia hali akiwa
hospitali kwani aliposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na nyota
huyo wa Argentina Jumatatu usiku.
Picha hiyo iliandikwa: ‘Asante
Carlitos kwa kunitembelea’.Tevez aliomba radhi mapema baada ya kutambua
maumivu ambayo amemsababishia Ham na akaamua kwenda kumtembelea
hospitali.
Kocha wa Argentinos Nestor
Gorosito alichelewa kukubali kwamba tukio hilo halikuwa la kukusudia kwa
kuangalia namna Ham alivyoumizwa.
Haikuwa bahati mbaya, Gorosito
aliiambia tovuti rasmi ya timu yak.Tulikuwa umbali wa mita tatu kutoka
eneo la tukio na tuliwea kuona…kwa waliocheza mpira wanajua haya mambo”


0 comments:
Post a Comment