10. Arjen Robben
Mchezaji
wa kimataifa wa Uholanzi Arjen Roben amekuwa ni moja ya wachezaji ambao
hawana nyota ya kutwaa tuzo licha ya kuwa na kiwango cha juu takribani
miaka 10 mfululizo. Anambinu nyingi, mchapakazi, maamuzi sahihi na kasi
ya ajabu nivitu ambavyo vinamfanya kuwa mchezaji hatari zaidi uwanjani.
Ameshashinda mataji yote
isipokuwa kombe la dunia ambalo timu yake ilishika nafasi ya pili mwaka
2010 nchini Afrika Kusini na wakawa watatu mwaka 2014 nchini Brazil.
Jina lake limekuwa likorodheshwa mara kadhaa kwenye orodha ya kuwania
mchezaji bora wa dunia FIFA Ballon d’Or lakini hajawahi kutwaa uzo hiyo.
Ni aina ya mchezaji ambaye
inapendeza kumtazama na huenda tukalitambua hilo baada ya kumaliza muda
wake wa kucheza soka miaka michache ijayo.
Medali ambazo Robben ameshatwaa hadi sasa
- Eredivise title
- Premier League title x2
- FA Cup
- Football League Cup x2
- La Liga title
- Bundesliga title x 3
- DFB- Pokal x 3
- Champions League
- UEFA Super Cup
- World Club Cup
9. Alessandro Del Piero
Del
Piero ni mchezaji anaekumbukwa kwa ufundi wake ‘master of his art’.
Juventus ilikuwa kama jukwaa la yeye kupigia show. Amekipiga ndani ya
Serie A, Champions League pamoja na kombe la dunia la mwaka 2006, enzi
zake akiwa na Maldini, Canavaro na Baggio palikuwa hapatoshi.
Kitu cha kushangaza ni kwamba,
hajawahi hata kukaribia kushinda tuzo ya Ballon d’Or. Alitakiwa kushinda
tuzo hiyo na wote tunajua hilo.
“Yeye ni tofauti na Zidane,
anapenda kucheza, anapenda kutoka moyoni; kati yake na mfaransa
(Zinedine Zidane) nasimama upande wake”, Diego Maradona.
8. Steven Gerrard
Wote
tunafahamu mafanikio ya legendary huyu wa Liverpool pale Anfield. Kitu
kikubwa cha kukumbukwa ni ubingwa wa Champions League wa mwaka 2005
ambao ulikuwa ni ubingwa wa kihistoria kwenye mchezo wa soka. Sio Legend
wa Liverpool pekee, bali ni EPL na mchezo wa soka kwa ujumla.
Alicheza kwa moyo wakati yupo
Liverpool na hakuona haya kuonesha wazi mapenzi yake kwa klabu yake.
Ukiangalia kwenye makabrasha ya rekodi huoni jina lake kwenye orodha ya
wachezaji waliowahi kutwaa tuzo kubwa.
“Amekuwa mchezaji mwenye ushawishi mkubwa England”, Sir Alex Ferguson.
“Kwa kazi aliyoifanya, ni miongoni mwa mashujaa”, Ronaldinho.
Mataji aliyoshinda Gerrard akiwa Liverpool
- FA Cup: 2001,2006
- Football League Cup: 2001,2003,2012
- FA Community Shield: 2006
- UEFA Champions League: 2005
- UEFA Cup: 2001
- UEFA Super Cup: 2001,2005
7. Raul Gonzalez
Kama
ilivyo kwa Ryan Giggs, ni vigumu kuelewa kwanini mkongwe wa Real Madrid
Raul Gonzalez hakunyanyua tuzo ya FIFA Ballon d’Or. Hadi sasa anabakia
kuwa mfungaji wa muda wote wa kikosi cha Los Blancos akiwa ametupia
kambani jumla ya magoli 323.
Ameifungia timu ya taifa ya
Hispania magoli 40, ameshinda UEFA Champions League mara tatu. Hakuwa
mchezaji mwenye mambo mengi uwanjani lakini mafanikio yake yalitosha
kumfanya ashinde tuzo hiyo.
“Nataka nimtakie nahodha kila
lakheri kwasababu alikuwa nguzo ya mafanikio kwa watu wengi na timu, na
amekuwa mtu ambaye watu wengi wanatakiwa kumtazama kwasababu
alichokifanya na alichokiamini. Asante kwake na kwa timu, na nakutakia
mema kwenye career yako”, David Beckham.
Medali za Raul akiwa Real Madrid
- Intercontinental Cup: 1998, 2002
- UEFA Champions League: 1997–98, 1999–2000, 2001–02
- UEFA Super Cup: 2002
- La Liga: 1994–95, 1996–97, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08
- Supercopa de España: 1997, 2001, 2003, 2008
6. Peter Schmeichel
Mashabiki
duniani kote watakubali kuwa, katika kipindi chake alikuwa ni golikipa
wa kiwango cha ajabu kuwahi kutokea kwenye mpira wa kisasa. Alishinda
mataji matano ya ligi na UEFA Champions league maarufu ya mwaka 1999.
Alikuwa ni golikipa mwenye kiwango ambacho iliwafanya wachezaji pinzani
wamuhofie golikipa huyu wa zamani wa kikosi cha Manchester United.
Ni
ngumu kuelewa ni kwanini Thiery Henry hakutwaa tuzao ya Ballon d’Or.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal mara kadhaa aliikaribia tuzo hiyo
lakini aliishia kuikosa mbele ya wachezaji kama Andriy Shevchenko mwaka
2004 licha ya ukweli kwamba alikuwa na mafanikio makubwa mwaka huo.
Rekodi za Henry zinafahamika
sana. Bado ni mchezaji pekee aliyehinda mara nyingi kiatu cha dhahabu
kwenye EPL. Mshindi mara tano wa tuzo ya chezaji bora wa Ufaransa,
mfungaji wa muda wote wa Arsenal, mchezaji mwenye magoli mengi kwenye
timu ya Ufaransa, na mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
ya FWA.
4. Paul Scholes
Ni
ngumu kwa mashabiki wa Manchester United kuamini kwamba kiungo wao
mahiri kwa miongo miwili amemaliza mpira wake bila kutwaa tuzo ya Ballon
d’Or. Bado anaonekana yuko fiti mara kadhaa ambazo anaonekana kwenye
mechi za wakongwe huku wengine wakisema bado alikuwa anauwezo wa kucheza
kwa miaka mingine kadhaa ijayo.
Lakini tayari mkongwe huyo hayupo
tena kwenye soka la ushindani na sehemu pekee unayoweza kumuona ni
kwenye uwanja wa mazoezi au kwenye majukwaa ya viwanja akiwa kama
mtazamaji.
“Kati ya wachezaji wote wa
Manchester United, ningemchagua Scholes-ni kiungo bora wa kizazi hiki.
Ningefurahi kucheza pamoja nae”, Pep Guardiola.
Medali alizowahi kutwaa Scholes
- Premier League (11): 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
- FA Cup (3): 1995–96, 1998–99, 2003–04
- Football League Cup (2): 2008–09, 2009–10
- FA Community Shield (5): 1996, 1997, 2003, 2008, 2010
- UEFA Champions League (2):1998–99, 2007–08
- Intercontinental Cup (1): 1999
- FIFA Club World Cup (1): 2008
3. Paolo Maldin
Hakuna
shaka kuwa huyu ndiye beki bora wa muda wote. Ameshinda kila taji
ambalo kwenye mchezo wa soka. Kutoka Serie A, Champions League hadi
kombe la dunia Maldini ameshinda yote. Japo Ballon d’Or ilimpitia
pembeni kwa muda wote aliocheza soka, mwaka 1994 alikuwa watatu nyuma
ya Hristo Stoichkov na Roberto Baggio.
Alishika namba tatu tena mwaka 2003 wakati huu akishindwa na Pavel Nedved. Ni aibu kwamba
Makombe ambayo Maldini ametwaa akiwa AC Milan
- Serie A (7): 1987–88, 1991–92, 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1998–99, 2003–04
- Coppa Italia (1): 2002–03
- Supercoppa Italiana (5): 1988, 1992, 1993, 1994, 2004
- European Cup/Champions League (5): 1988–89, 1989–90, 1993–94, 2002–03, 2006–07
- UEFA Super Cup (5): 1989, 1990, 1994, 2003, 2007
- Intercontinental Cup (2): 1989, 1990
- FIFA Club World Cup (1): 2007
2. Ryan Giggs
Alilipendezesha soka la England
katika historia ya soka. Alicheza mechi 963 akiwa na Manchester United
akifanikiwa kushinda mataji 34. Sababu za kwanini Giggs hajawahi
kushinda tuzo ya Ballon d’Or ni kitendawili ambacho hakijapatiwa majibu
hadi sasa.
Watu wengine wanaweza kusema
Giggs hana historia nzuri akiwa na timu yake ya taifa lakini
wanasau Andriy Shevchenko alitwaa tuzo hiyo mwaka 2004 huku akiwa hana
historia hata ya kukaribia kushinda taji lolote akiwa kwenye timu ya
taifa.
Mafanikio aliyopata Giggs akiwa Manchester United
- 963 games for Manchester United
- 672 league appearances
- 151 Champions League appearances
- 109 league goals
- 45 opponents in the Premier League
- 34 trophies
- 13 Premier League titles
- 4 FA Cups
- 2 Champions Leagues
- 1 club World Cup
1. Xavi Hernandez
Ukweli
kwamba Xaxi Hernandez kutoshinda FIFA Ballon d’Or ni aibu si kwa FIFA
na UEFA pekee bali ni aibu kwa soka kwa ujumla. Watu wengi wanasema
kwamba, Messi billa Xavi na Iniesta anakuwa mtu mwingine tofauti kabisa.
Alikuwa ni injini ya timu kwa miaka mingi. Alikaribia kutwaa tuzo hiyo
lakini haikuwezekana.
Johan Cruyff: “Kama Xavi
asipokuwa sawa basi Barcelona haitacheza vizuri kwa kiwango kilekile
kama ilivyozoeleka. Ni mtu ambaye anamiliki na kuamua mchezo. Kucheza
kwake kunairuhusu timu kucheza. Yuko tofauti”.
Medali ambazo Xavi amevaa akiwa Barcelona- La Liga: 1998–99, 2004–05, 2005–06, 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2012–13, 2014–15
- Copa del Rey: 2008–09, 2011–12, 2014–15
- Supercopa de España: 2005, 2006, 2009, 2010, 2011, 2013
- UEFA Champions League: 2005–06, 2008–09, 2010–11, 2014–15
- UEFA Super Cup: 2009, 2011
- FIFA Club World Cup: 2009, 2011
- International
- FIFA World Cup: 2010
- UEFA European Football Championship: 2008, 2012
- Summer Olympics Silver Medal: 2000
- FIFA Confederations Cup Silver Medal: 2013
- FIFA World Youth Championship: 1999
0 comments:
Post a Comment