Alizaliwa
katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu Harare,
alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza
katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.
Yafuatayo
ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa wayajua kumhusu kiongozi huyu-na
ambayo huenda yamemuwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno.
Mugabe akionekana mwenye furaha mno
1) Zoezi na vyakula vya kienyeji
Mugabe
anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya
mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu
iliyopita. Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na
kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia.
Siri
nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa ywapenda sana-chakula
cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila
hunywa pombe kidogo anapokula.
Mugabe akiwa na familia yake.
2) 'Kufufuka'
Ingawa
kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na
kazi yake ya kisiasa yaendelea vyema kabisa. Kuhusu afya yake Mugabe
alipohojiwa wakati mmoja alisema,“ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo
humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,”
alisema alipotimia miaka 88.
Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-mamake alikuwa mcha
Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC,
miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa
sana.
3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi
Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi.
Ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba
yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare, ambapo anaweza kutazama kwa
makini wakati wa michezo wa kitaifa.
“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa
wema,” Bw. Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia
uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe
iwe nchi ya wangwana.”
4) Hapendi kushindwa
Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika
mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki
alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi
yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko
Uingereza na Uhispania mtawalia. “ Ninapotazama kandanda, sitaki
usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012. “Hata mke wangu
anajua mahala pa kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia
hufunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele
yangu.”
5) Alipata mtoto akiwa miaka 73
Ana watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani
wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao
kufunga ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa
miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe alinyimwa ruhusa ya kuenda
Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa
kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.
6) Anampenda Cliff Richard kuliko Bob Marley
Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere,
alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha
kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Bw. Mugabe hakumtaka
muimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji
maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na waimbaji wa mitindo
ya reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini Jamaica, wana uhuru wa
kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote wamelewa. Hawataki kuenda
shule; wanataka tu kuimba, na kufuga rasta. Kama Zimbabwe, tusielekee
hapo.”
7) Mvaaji wa nguo maridadi
Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake visawasawa na tai
zinazofanana na kitambaa. Hwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa
mavazi yake. Ila, mwanamitindo ambaye humshonea nguo zake ,Khalil
Parbhoo anasema: “Bado huavlia kama mabwana wa Uingereza –hivyo ndivyo
anavyopenda."
8) Anamtzama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia
uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe
alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na
kuiongoza Ghana kupata uhuru;Kwame aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa
Ghana haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”
9) Ni mtu mwenye shahada nyingi
Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka
katika chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii
zake zingine kwa njia Internet-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za:
elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Amejitapa kuwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama
vya kutetea haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia
kugoma.
0 comments:
Post a Comment