Michuano ya FA Cup ambayo mwaka huu na miaka minne inayofuata itajulikana kwa jina la Azam Sports Federation Cup, si mipya katika soka la Tanzania. Miaka ya nyuma FA Cup ilikuwepo na kwa mara ya mwisho ilichezwa mwaka 1997.
Tanzania Stars chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ndio ilikuwa timu ya mwisho kuchukua ubingwa huo na kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Mashindano haya kwa mwaka 2015/16 yatashirikisha jumla ya timu 64 kutoka ligi kuu (VPL), ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili. Kutakuwa na raund saba toka kuanza kwa mashindano hadi kumalizika kwake.
Mashindano yataanza mwezi Novemba kwa raundi ya kwanza na yataendelea mpaka mwezi Mei 2016 ambapo ndio utapigwa mchezo wa fainali. Bingwa wa FA Cup msimu huu atawakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho.
Utaratibu ulioandaliwa ni kwamba, kuanzia mwezi Novemba kutakuwa na wiki maalumu ya FA Cup ambayo itakuwa ni rasmi kwa michezo inayohusisha FA Cup ambayo itachezwa kwa njia ya mtoano na timu itakayokuwa inashinda itapata nafasi ya kucheza round inayofuata.


0 comments:
Post a Comment