Mwenyekiti wa National Governance Internet Forum ambaye pia ni
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya
akiwakaribisha wadau wa mitandao na watumiaji wa intaneti kwenye jukwaa
hilo kabla ya kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA
kufungua rasmi jukwaa hilo.. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tanzania
Education and Research Network (TERNET), Amos Nungu na Kushoto ni Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akifuatiwa
na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Bw. Sunday Richard. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Bw. Sunday Richard akifungua rasmi Jukwaa la wadau wa usimamizi
wa masuala ya mtandao (NIGF) lililoandaliwa na Umoja wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kufanyika mwishoni mwa juma
katika ukumbi wa mikutano COSTECH jijini Dar. Kushoto ni Ofisa Miradi ya
Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliyemwakilisha Mkurugenzi
wa UNESCO na kulia Mwenyekiti wa National Governance Internet Forum,
Kenneth Simbaya.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph
aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO akitoa salamu za shirika la UNESCO
wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao
(NIGF) ulioandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania
(UTPC).
Katibu Mtendaji wa Tanzania Education and Research Network
(TERNET), Amos Nungu akitoa salamu za TERNET kwa wadau waliohudhuria
jukwaa hilo.
Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh akiwasilisha mada
iliyoelezea umuhimu wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo wakati wa
jukwaa hilo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki waliohudhuria jukwaa
hilo wakifuatilia "presentation" iliyokuwa ikitolewa na Mtaalamu kutoka
TCRA Dk. Emmanuel Manasseh (hayupo pichani).
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph
kwa mtaalamu kutoka TCRA (hayupo pichani) kama wana mipango gani
kuhakikisha kuwa kutakuwepo na masafa ya kutosha kwa miaka mingi ijayo
kwaajili ya wananchi wa vijijini na wale wasio na uwezo.
Picha ya pamoja.
Maxence Melo kutoka Jamii Forum akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa jukwaa lililowakutanisha kwa pamoja wadau wa masuala ya
mitandao ya intaneti.
Maxence Melo kutoka Jamii Forum (katikati) akipata picha ya
pamoja na wajumbe wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Fredy Njeje wa
Blog za Mikoa (kulia) na Mr. Verbs.


0 comments:
Post a Comment