https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    UNHCR LIMEONYA KUWA MAELFU YA WAKIMBIZI WATAACHWA NJIA PANDA ULAYA

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) limeonya kuwa maelfu ya wakimbizi wataachwa njia panda kufuatia nchi za Umoja wa Ulaya kuamua kutumia sheria tofauti za kudhibiti mipaka ili kukabiliana rekodi ya idadi kubwa ya wahamiaji.

    Kauli hiyo ya UNHCR imekuja wakati Ujerumani ikianzisha udhibiti katika mpaka wake na nchi ya Austria.

    Shirika hilo limetoa wito wa kuanzishwa kwa kituo kikubwa cha Umoja wa Ulaya cha kuwapokea wahamiaji wanaowasili mataifa ya Ulaya.

    Wakati huo huo Mawaziri wa Mambo ya Ndani wa Ulaya, wanafanya mkutano wa dharura hii leo kujadili namna ya kukabiliana na mgogoro wa wahamiaji.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UNHCR LIMEONYA KUWA MAELFU YA WAKIMBIZI WATAACHWA NJIA PANDA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top