Meneja wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu muhandisi
Justus Mtolela amesema kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha megawati
mia mbili kimepunguza uzalishaji wake hadi kufikia megawati 30 na kwamba
hali hiyo inatokana na kukosekana kwa maji ya kuendeshea mitambo ambapo
kina cha maji katika bwawa la Kidatu kimeshuka kutoka mita za ujazo 450
hadi kufikia mita 441 huku kiwango cha mwisho kinachoruhusiwa kuzalisha
umeme kikiwa ni mita 433.
Kukauka kwa maji katika bwawa la Mtera na Kidatu ni athari
inayotokana na kukauka kwa maji ya mto Ruaha mkuu ambao ndiyo tegemeo la
bwawa hilo la Mtera linalohudumia pia bwawa la Kidatu kwa pamoja na mto
Lukosi na Iyovi ambayo na yenyewe imekauka.
Hivi karibuni baadhi ya wataalamu na wadau wa rasilimali za maji
wamekuwa na maoni na mapendekezo kwa serikali juu ya hatua zinazopaswa
kuchukuliwa ili kunusuru rasilimali hiyo na kuifanya kuwa endelevu ikiwa
ni pamoja na kutazama upya mgawanyo wa maji kwa sekta mbalimbali na pia
kusimamia ufanisi katika matumizi yake.
0 comments:
Post a Comment