Dereva wa mbio za magari za
Langlanga Carlos Sainz atashiriki mbio za magari za Russia Grand Prix
hii leo, licha ya kupata jali wakati wa mazoezi.
Dereva huyo Mhispania alikimbizwa
hospitali huko Sochi, baada ya kugonga uzio katika kona ya 13, akiwa
katika mwendo kasi, hata hivyo aliruhusiwa kutoka hospitali jana.
Shirikisho linalosimamia michuano ya
mbio za magari za Langalanga FIA, limemruhusu Sainz kushiriki mbio za
magari baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari.
Kampuni ya Toro Rosso imelifanyia
matengenezo gari la Sainz jana usiku na imethibitisha kuwa dereva
huyo atashiriki mbio hizo za Russia Grand Prix.
0 comments:
Post a Comment