https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    WAFANYAKAZI BOA BENKI KUPEPERUSHA BENDERA YAO NA CCBRT MLIMA KILIMANJARO KUANZIA JUMAPILI HII


    Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wanao kwenda kupeperusha bendera ya benki hiyo pamoja na bendera ya CCBRT katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro ikiwa ni kukamilisha mchango wao kama benki kwaajili ya watoto waliozaliwa ikiwa miguu yao imepoza ili wapatiwe matibabu katika Hospitali ya CCBRT, ikiwa ni mchango wao kama benki kusaidia jamii inayosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda miguu unaojulikana kwa jina la (KIBWIKO) benki ya BOA imekusanya kiasi cha USD 100,000  kwaajili ya kuchangia matibabu ya wanaopatwa na matatizo hayo, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo.
    Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya BOA ambao wateenda kupererusha bendera ya benki hiyo pamoja na bendera ya hospitali ya CCBRT katika kilele cha mlima Kilimanjaro  kuanzia jumapili hii. 
     Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi .
     Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera ya BOA benki Mwenyekiti wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam.
     Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera ya Hospitali ya CCBRT Mwenyekiti wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam, ambapo itatia moyo kwa makampuni binafsi kuchangia jamii kama walibyofanya benki hiyo.
    Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera yenye nembo ya BOA benki  pamoja na nembo ya Hospitali ya CCBRT Mwenyekiti wa msafara wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam,ikiwa Mkurugenzi huyo akiwatakia kila raheri wafanyakazi wa benki hiyo kufanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kurudi wakiwa na kumbukumbu kwao pamoja na ushindi katika jamii ikiwa ni faida na hata kwenye afya zao kwa ujumla alisema.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAFANYAKAZI BOA BENKI KUPEPERUSHA BENDERA YAO NA CCBRT MLIMA KILIMANJARO KUANZIA JUMAPILI HII Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top