Katibu
wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani (wa pili
kushoto), akipokea fomu ya usajili kutoka kwa Katibu wa chama cha riadha
Mwanza, Peter Mujaya (wa pili kulia), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita
tano katika mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15
Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wanaoshuhudia
ni Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Mwanza, Kizito Bahati (kushoto) na
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus
International, Bi. Adella Lamsa (kulia).
Katibu
wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani, akisaini
fomu ya usajili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana
alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za
Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015
katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Kaimu Afisa
Michezo mkoa wa Mwanza, Kizito Bahati (kushoto) na Katibu wa chama cha
riadha Mwanza, Peter Mujaya (kulia).
Katibu
wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani (kushoto),
akionyesha fomu ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi
kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za Rock City
Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kulia ni mwakilishi wa New Mwanza Hotel
ambao ni moja wa wadhamini wa mbio hizo, Senthil Kumar na Katibu wa
chama cha riadha Mwanza, Peter Mujaya (wa pili kulia).
Katibu
wa idara ya utumishi Mwanza, Genzi Sahani, akisoma risala ya Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, jana jijini Mwanza muda mfupi kabla ya
kuzindua usajili wa washiriki wa mashindano ya Rock City Marathon mbio
za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015
katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mratibu
wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus
International, Bi. Adella Lamsa, akiongea wakati wa uzinduzi wa usajili
wa washiriki wa mashindano hayo jijini Mwanza jana ambapo Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Magesa Mulongo, alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za
kilomita tano zitakazofanyika Novemba 15, 2015 katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Meneja
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Mwanza, Shaaban Luanda,
akiongea wakati wa uzinduzi wa usajili wa washiriki wa mashindano hayo
jijini Mwanza jana ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo,
alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano
zitakazofanyika Novemba 15, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Na mwandishi wetu
Ikiwa
ni siku chache kupita baada ya uzinduzi wa mbio za Rock City Marathon
2015, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo amekua mtu wa kwanza
kujisajili kushiriki mbio hizo zilizopangwa kufanyika Novemba 15 mwaka
huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizindua
usajili wa ushiriki wa mbio hizo jijini Mwanza jana, Mulongo,
aliyewakilishwa na Katibu idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza,
Bw. Genzi Sahani, alitoa wito kwa wanariadha nchini kujitokeza kwa
wingi ili kuongeza ushindani wa mbio za mwaka huu, ambazo zimekuwa na
lengo la kuhimiza utalii wa ndani nchini.
“Nimekuwa
mfuatiliaji wa mbio hizo tangu zilipoanzishwa mwaka 2009 na
tumeshuhudia viwango vya mbio hizi vikipanda kila mwaka, kitu ambacho ni
kielelezo cha kuonyesha maandalizi mazuri yanayofanywa kwa kuzingatia
viwango na sheria zilizo wekwa,” alisema Mulongo katika shughuli hiyo
iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha.
Mulongo,
alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni mchezo wa riadha umekua
ukififia na kutaka wadau mbalimbali, ikiwemo makampuni binafsi,
kuunganisha nguvu ili kuurudisha kwenye ramani mchezo huo ulioliletea
taifa sifa kubwa katika miaka ya nyuma.
“Ni
kweli kwamba makampuni na hata watu binafsi wanajitokeza kusaidia kukuza
mchezo wa riadha hapa nchini, lakini bado mchezo huu una changamoto
nyingi hususani katika mkoa wetu wa Mwanza na bado zinahitajika jitihada
za ziada kwa wadau mbali mbali wa mchezo huu kushirikiana ikiwa ni
pamoja na makampuni binafsi bila kusahau viongozi wa chama cha Riadha
Mkoani Mwanza,” alisema.
Akizungumza
katika shughuli hiyo, Meneja wa Shirika la hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa
wa Mwanza Shaaban Luanda, ambao ni wadhamini wakuu, alisema: “Mbio za
Rock City Marathon zimekuwa na mchango mkubwa katika kuinua mchezo wa
riadha nchini. Sisi kama shirika la hifadhi ya jamii tunaamini kupitia
michezo tunaweza kulinda afya ya jamii na ndio maana tumeendelea
kudhamini mbio hizi.”
0 comments:
Post a Comment