Timu ya taifa ya Wales ikiongozwa
vyema na nyota wao Gareth Bale imefanikiwa kutinga michuano ya Euro
2016 licha ya kikosi chao kinachonolewa na kocha Chris Coleman
kufungwa jana usiku.
Wales imefanikiwa kufuzu kuingia
katika michuano hiyo jana usiku kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958,
hata baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Bosnia katika mchezo
uliochezwa kwenye dimba la Bilino Polje.
Katika mchezo huo Bosnia iliandika
bao la kwanza kupitia kwa Milan Djuric kwa kichwa cha kunyanyua mpira
juu na kumpita Wayne Hennessy, ambapo Vedad Ibisevic aliipachikia
Bosnia bao la pili.
Furaha ya kufuzu Euro 2016, Bale na wenzake wakitereza uwanjani
Kocha Chris Coleman akibebwa juu juu na wachezaji wa Wales
0 comments:
Post a Comment