Msafara wa magari ya wanajeshi wa
Uingereza umeshambuliwa ukiwa katika dori katika Jiji la Kabul nchini
Afghanistan.
Wizara ya Ulinzi wa Uingereza
imesema shambulio hilo limetokea katika eneo la makazi ya watu karibu
na soko hii leo na kujeruhi watu saba. Hakuna Muingereza
aliyejeruhiwa.
Wapiganaji wa Taliban wamesema
wamefanya mashambulizi hayo kujibu mapigo ya mashambulizi ya anga
yaliyofanywa katika mji wa Kunduz yaliyouwa raia na madaktari.
0 comments:
Post a Comment