Benki ya CRDB kupitia
tawi lake la mjini Geita imechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika Shule za Msingi Mwatulole na Shule ya Msingi Geita ambayo baadhi
ya majengo yalibomolewa na mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali
mwanzoni mwa mwake huu mkoani Geita.
Sambamba
na kusaidia ujenzi na ukarabati wa madarasa Benki ya crdb ilichangia
maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika mjini
Geita kwa sababu benki hiyo inawajali wateja wake. Maadhimisho ya wiki
Huduma kwa Wateja ilianza Oktoba 5 na kumalizika Oktoba 10 ambapo Benki
ya CRDB ilishiriki kikamilifu katika kazi za kijamii. Benki ya CRDB imewashuru wateja wake kupitia tawi la Geita.
Meneja wa CRDB Geita, Amini
Mwakang'ata (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja Mkuu
wa Shule ya Msingi Mwatulole iliyopo Mkoani Geita, Catherine Mugusi kwa
ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.

Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto) akipokea
maoni kutoka kwa mteja wa wa Benki ya CRDB tawi la Geita wakati wa
Maadhiisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mjini Geita.
Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akizungumza na
wateja wa benki hiyo (hayupo pichani) katika maadhimisho ya Wiki ya
Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Geita.
0 comments:
Post a Comment