Kampuni
ya Connectmoja Technologies inayoendesha
shughuli zake hapa nchini Tanzania leo imezindua Mfumo madhubuti unaojulikana kwa
jina la KSchool Management system.
Akizungumza
na wana habari, Mtaalamu wa utafiti na ukuzaji wa Masoko Bw. Fred Crich
amewaambia wanahabari kwamba Kampuni yao ya ConnectMoja Technologies imejikita zaidi katika kuhakikisha inasaidia
sekta ya elimu na uwekezaji kukua pamoja na maendeleo ya Teknolojia hapa
Nchini.
Bw. Crich amesema mfumo huu umewalenga wamiliki wa mashule kwani
mfumo unawawezesha kuweka rekodi sahihi za wanafunzi, kutunza kumbukumbu za
mienendo ya wanafunzi, kuweka rekodi ya matokeo ya wanafunzi na wazazi pia
wanaweza kuona rekodi hizi wakiwa majumbani au mahala popote kwa kutumia simu
za kiganjani au computer zenye internet; Mfano. Mwanafunzi anapotoka shule, Mzazi atakuwa na uwezo wa
kuingia kwenye mfumo huu kupitia(Parent
Portal) na kujua kama mtoto alifika shuleni, na kama alifika alifundishwa nini,
pia kujua kama ana Homework ya kufanya pindi afikapo nyumbani, pia itamwonesha
matokeo yake papo hapo.
Mfumo
huu una Teachers Portal na students portal ambapo Mwalimu anaweza kutuma
Assignments kwa wanafunzi hata wakiwa Likizo.
Bw.
Crich ameelezea kwamba mfumo huu umeanza kutumika kwenye baadhi ya shule hapa
Nchini na kwa sasa wameuboresha zaidi ili uweze kuwanufaisha wazazi pamoja na
wadau wa sekta ya elimu.
Pia
anakaribisha wamiliki wa shule wote wanaotaka kuupata mfumo huu, bei ni nafuu .
Kwa
maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:
call: +255 777 88 0000 7 au
0714 215 600
0 comments:
Post a Comment