Kwa sababu kila mtu anahitaji kuwa na
kifaa kizuri cha Mawasiliano, nimeona kuna umuhimu pia uipate na hii
mpyampya kutoka Kampuni ya Kampuni ya Microsoft, Marekani.
Microsoft
ni kampuni ambayo imewekeza sana kwenye Teknolojia, walianza na
biashara ya kutengeneza program za Computer, baadae wakaendelea kukuza
biashara yao… mwaka 2014 Microsoft waliamua kuinunua pia Kampuni ya Nokia na kuendelea na Biashara ya uzalishaji wa Simu.
Kipya kinachokuja ni hii laptop mpya, imepewa jina la Microsoft Surface Book,
hii ni zaidi ya laptop ya kawaida, ina uwezo wa kutumika kama Laptop au
unaitenganisha alafu unaendelea kuitumia kama Ipad pia… hii itakuwa ya
kwanza kabisa kutengenezwa na Kampuni hiyo ya Microsoft.
Unaambiwa kama ikijaa chaji ina uwezo wa
kufanya kazi mpaka kwa saa 12, mpango walionao ni kuitambulisha na
kuiingiza rasmi sokoni kuanzia October 26 2015 na itauzwa kwa Dola 1,499
ambazo zinagusa kama Milioni 3.2.
Iko na video yake pia hapa kwenye sekunde 96.
0 comments:
Post a Comment