Meneja Mwandamizi
wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB, Haika Machaku
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuwapatia shuhulisho
la masuala ya kifedha wateja na kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara zao
ameyasema hayo leo katika hafla ya kusherekea wiki ya huduma kwa wateja
iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa
Technolojia ya Habari na mawasiliano Mohamed MtuliaMeneja Mwandamizi
wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB, Haika Machaku akikata
keki na wateja wa Benki hiyo katika hafla ya kusherekea wiki ya huduma
kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
BENKI ya DCB leo
imezindua wiki ya huduma kwa wateja wake ikiwa ni moja ya hatu za kuonesha
inawatambuwa, kuwashukuru na kuwajali. Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Haika Machaku amesema wanajivunia kuwa
sehemu ya maendeleo ya wateja wao kutokana na mikopo waliyoanza kuitoa tangu
mwaka 2008 iliyowezesha wananchi kununua viwanja na kujenga nyumba.
Machaku amesema
kauli mbiu ya benki hiyo kwa mwaka huu ni ‘Tupo kwa ajili yenu’ ambayo
inadhihilisha lengo lao juu ya utoaji wa huduma bora zenye staha na kukidhi
matakwa ya wananchi.
Amesema katika kuhakikisha huduma bora kulingana na mahitaji ya wateja wao, wameweka njia nyingi za mawasiliano yaliyowezesha kupokea maoni kutoka kwa wateja.
“Pamoja na
kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja ya mwaka huu pia tumeboresha huduma ya
mikopo kwa wateja wetu. Kwa sasa wanaweza kupata mikopo ya nyumba kwa gharama
nafuu sana,” amesema Machaku.
Mmoja wa wateja
wa benki ya DCB, Mwajuma Kombo amesema huduma za benki hiyo ni nzuri na
zinawasaidia katika kutatua mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kujenga
nyumba na kununua nyumba pia kupitia mikopo inayotolewa.
Kombo amewashukuru watendaji wa benki hiyo kwa kuanzisha wiki
hiyo ya huduma kwa wateja kwani inaonyesha ikuwa benki hiyo inawajari wateja
wake.
“ Nimejiunga na
benki ya DCB tangu ilipoanza kutoa mikopo mwaka 2008 hadi sasa na mambo mengi
nimeweza kuyafanya kupitia mikopo hiyo ikiwemo kusomesha watoto na kujenga
nyumba yangu mwenyewe.” amesema Kombo.
|
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment