Oscar Pistorius akiwa mahakamani.
MWANARIADHA mlemavu wa nchini Afrika
Kusini Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu
baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake
Reeva Steenkamp mnamo mwaka 2013.
Wazazi wa Reeva Steenkamp wakiwa mahakamani.
Pistorius ameachiliwa
huru usiku wa kuamkia leo na kuamliwa kutumikia kifungo cha nje hadi
pale atakapomaliza kifungo hicho cha miaka mitano.
Baada ya kuachiliwa huru, alielekea kwa mjomba wake Arnold Pistorius.
Oscar Pistorius akiwa na aliyekuwa mpenzi wake marehemu Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo alipatikana hatia mwezi Octoba mwaka ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Kama sehemu ya msamaha huo, bingwa huyo
wa zamani wa mbio za walemavu atahitajika kukaguliwa kisaikolojia kila
baada ya kipindi fulani na hataruhusiwa kumiliki bunduki tena.
…Akisikiliza hukumu.
Familia yake imekanusha madai kuwa
ameachiliwa mapema ikisema kuwa japo hayumo gerezani angali anatumikia
kifungo chake nyumbani.
Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa
hajapunguziwa kifungo na atatumikia kipindi hicho kwa uadilifu kulingana
na sheria za taifa.
Hata
hivyo bingwa huyo wa zamani anakabiliwa na hatari ya kurejeshwa
gerezani iwapo kiongozi wa mashtaka atafaulu kubatilisha uamuzi wa
mahakama ya chini iliyompata na hatia ya kuua bila kukusudia Steenkamp.
0 comments:
Post a Comment