Mshambuliaji wa Chelsea Diego
Costa ametajwa kuwa mchezaji mwenye tabia chafu zaidi katika ligi kuu
Uingereza msimu huu, baada ya kuondoka kwa Mario Baloteli na Joey
Barton.
Lakini mbali na Costa hii ndio
listi ya wachezaji wengine waliowahi kuwa na tabia kama hizo kuwahi
kutokea katika historia ya EPL katika nyakati tofauti tofauti.
5. Scott Parker
Kiungo huyu wa Kiingereza
amejikusanyia kadi takribani 86 za manjano katika muda wote aliocheza
ligi kuu Uingereza akiwa na vilabu vya Chelsea, Newcastle United, West
Ham United,Tottenham Hotspur na Fulham(kabla haijashuka daraja).
4. Patrick Vieira
Alisajiliwa na Arsenal akitokea
kunako klabu ya Inter Milan, kiungo na nahodha huyo wa zamani wa
Arsenal, alikuwa ni mpinzani mkubwa wa nahodha wa zamani wa Manchester
United Roy Keane ambaye pia alisifika kwa tabia chafu.
Licha ya kubeba makombe matatu
ya EPL likiwemo lile ambalo walimaliza ligi bila ya kufungwa , Vieira
ndiye nahodha pekee wa Ligi Kuu Uingereza kupata kadi mbili za manjano
katika matukio sita kwenye mchezo mmoja na kuonyeshwa kadi mbili
nyekundu. Katika kipindi chote cha maisha yake ya soka Vieira alipenda
sana migongano na wachezaji wenzake kama Roy Keane.
3. Kevin Davies
Huyu ni nahodha wa zamani wa
Bolton Wanderers amefanya na kufanyiwa faulo nyingi zaidi katika
historia ya Ligi Kuu nchini Uingereza.
Alicheza katika klabu kadhaa katika miaka yake 22 ya maisha yake ya soka zikiwemo Southampton, Bolton Blackburn Rovers.
2. Paul Scholes
Kiungo huyu wa zamani wa
Manchester United ni mchezaji wa tatu kwa kuonyeshwa kadi za njano
nyingi zaidi katika historia ya Ligi Kuu Uingereza nyuma ya mshambulizi
wa zamani wa Bolton Kevin Davies na kiungo wa zamani wa Newcastle Lee
Boywer.
1. Vinnie Jones
Huyu unaweza kumwita mchezaji
mgumu kuliko kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka, Jones anashikilia
rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kupewa kadi kwa haraka zaidi
katika mchezo rasmi, akipewa kadi baada ya sekunde tatu tu kwenye mchezo
wa kuwania kombe la FA mwaka 1992 wakati akikipiga kunako klabu ya
Chelsea.
Jones ametolewa nje katika
matukio sita tofauti katika Ligi Kuu nchini Uingereza, akizawadiwa jumla
ya kadi nyekundu 12 katika maisha yake yote ya soka na kufunga ukurasa
wa wachezaji wenye nidhamu mbovu zaidi katika mchezo wa soka kunako Ligi
Kuu Uingereza .
0 comments:
Post a Comment