Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete akiingia katika Ukumbi wa Mlimani City tayari kwa hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) jana jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia) akizungumza na rais wa zamani wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga (katikati) katika sherehe ya kumuaga Rais Kikwete iliyoandaliwa na Taswa juzi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
Nahodha wa Taifa Stars na Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (katikati) akiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto katika hafla hiyo.
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (katikati) akiteta jambo na mwandishi mkongwe wa habari za michezo, Said Salum (kulia), kushoto ni Baruhan Muhuza wa Azam TV.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (kushoto) akizungumza na Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa (katikati) katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete jana kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Bondia Cosmas Cheka (kulia) akiwa kwenye hafla ya kumuaga Rais Kikwete jana kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Kipindi cha ‘The Mboni Show’, Mboni Masimba (kulia) akiwa na mdau katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Mkurugenzi wa Lino Agency waandaaji wa Miss Tanzania, Hashimu Lundenga (katikati) akiteta jambo na mmiliki wa sufianimafoto blogspot, Sufian Mafoto (kulia). Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taswa, Mroki Mroki.
Rais Kikwete (kushoto) akimkabidhi tuzo Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kutambua mchango wake katika soka muda wote wa miaka kumi ya utawala wake.
Rais Kikwete (kushoto) akikabidhi tuzo kwa bondia Francis Cheka jana usiku kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akipokea tuzo ya kuthamini mchango wake kwa wanamichezo Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto kwenye hafla ya kumuaga raia jana usiku kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) jana usiku kilifanya sherehe ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam pia kumpa tuzo maalum ya kuheshimu mchango wake katika michezo kwa kipindi cha miaka kumi madarakani.
Katika sherehe hiyo, Rais Kikwete alikabidhi tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwenye kipindi chote cha utawala wake.
PICHA: MUSA MATEJA/GPL
0 comments:
Post a Comment