https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    JAJI MKUU ATAKA SWALA LA KULINDA KURA MITA 200 LIACHIWE MAHAKAMA IAMUE

    Wakati Mbowe akisisitiza msimamo wa kuwataka wafuasi wa Ukawa kutorudi nyumbani baada ya kupiga kura na badala yake kukaa umbali wa mita 200 kutoka vituo vya kupigia kura ili kulinda kura zao, Jaji Mkuu Othman Chande alikataa kuzungumzia suala hilo na badala yake kutaka mahakama iachiwe ili itoe uamuzi wake kwa haki.
    Jaji Chande aliyasema hayo jana wakati alipoulizwa na waandishi baada ya kufungua mafunzo kwa majaji na Wasajili Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam, juu ya wajibu wa mahakama katika uchaguzi mkuu na namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika kusimamia kesi za uchaguzi, yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).
    Tayari Mahakama Kuu imeshapanga majaji watatu kushughulikia suala hilo lililoibua mvutano mkali hivi karibuni baina ya viongozi wa Ukawa na wakuu wa Nec na Jeshi la Polisi. Kesi hiyo itaanza kunguruma rasmi leo. 
    Katika hatua nyingine, Jaji Chande alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wenye mchuano mkali na kwamba mahakama zimejiandaa kumaliza kesi zitakazotokana na uchaguzi huo kabla ya miezi sita inayotajwa kisheria.
    Alisema mwaka 2010 kulikuwa na kesi 44 za uchaguzi kwa ngazi za Ubunge na kati yake, 17 zilikwenda hadi hatua ya mwisho baada ya kutolewa ushahidi huku nyingine zikiisha katika hatua za awali.
    “Ushindani ni mkali katika uchaguzi huu, tunatarajia kupokea kesi nyingi za uchaguzi. Tumejiandaa kupokea, kusikiliza kwa haraka ili kuwezesha wapigakura kujua mshindi halali ni yupi,” alisema.
    Akieleza zaidi, alisema sheria imeweka wazi kuwa anayestahili kufungua kesi siyo mpigakura bali wagombea wenyewe.
     
    Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa, alisema wameshirikiana na Ofisi ya Jaji Kiongozi kuandaa mafunzo hayo kwa kutambua kuwa ni wadau muhimu katika kushughulikia kesi za uchaguzi ili kuwezesha haki kutendeka kwa haraka

    Goodluck Jonathan  Akiri  Ushindani  Ni  Mkali  Kati  Ya  CCM na  UKAWA
    Mkuu wa Jopo la Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amekiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu nchini Tanzania una ushindani mkali kutokana na namna vyama vilivyojiandaa lakini akawataka wagombea wote wa nafasi za urais kujiandaa kukubali matokeo kwa maslahi mapana ya taifa lao.
     
    Wagombea wanaochuana kwa karibu ni, Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Lowassa.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini, Jonathan aliyekubali kuondoka madarakani Mei mwaka huu na kumpisha Muhammad Buhari baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu nchini mwake, alisema katika uchaguzi wowote kuna kushinda na kushindwa na hivyo wagombea wajiandae kwa matokeo yoyote ili kuiacha nchi yao ikiwa salama.

    Alisema ijapokuwa ushindani ni mkali, Jumuiya ya Madola inaamini kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba imani yao kubwa ni Tanzania kusimamia demokrasia iliyokuwapo wakati wote tangu ipatre uhuru wake mwaka 1961.
    Jonathan anaongeza jopo lenye waangalizi 14 kutoka mataifa mbalimbali yaliyo wanachama wa Jumuiya ya Madola
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JAJI MKUU ATAKA SWALA LA KULINDA KURA MITA 200 LIACHIWE MAHAKAMA IAMUE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top