Mkurugenzi
Mkuu wa mradi huo Uhuru One, Rajab Katunda (kushoto), akizungumza
katika mkutano huo kuhusu mradi huo. (katikati) ni Meneja Mradi huo wa
Tigo, Kobbina Awuch.
Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo
kutoka Uhuru One, Rajab Katundu wakifuatilia mkutano huo.Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab Katunda wakiwa katika picha ya pamoja.
Meza kuu.
Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uhuru One, Baraka Mtunga,
Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab Katunda, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez na Meneja Mradi huo wa Tigo, Kobbina Awuch
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Tigo imeanzisha mfumo wa kuunganisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wa
mtandao huo na wakazi wa Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha
mawasiliano.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo,
Diego Gutierrez alisema upanuzi wa 4G umetokana na mafanikio
yaliyopatikana katika awamu ya majaribio yaliyofanywa na kampuni hiyo
maeneo ya Mliman Cioty na Masaki Peninsula April mwaka huu.
Alisema
upatikanaji wa 4G jijini kote unaridhisha na kwamba dhamira ya tigo ni
kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini na kuongoza katika utoaji wa
huduma zaidi na za uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa wateja.
Gutierrez
alisema mtandao wa 4G LTE unamaanisha ongezeko la kasi ya kuperuzi na
kupakua habari kutoka kwenye intaneti, kupiga simu kwa njia ya skype.
pia inamwezesha mteja kupata mtiririko wa video au kufanya mkutano kwa
njia ya mtandao kwa ubora wa hali ya juu.
"Upanuzi
huu unamaanisha wateja wa tigo waliopo katika wilaya za Kinondoni, Ilala
na Temeke waishio maeneo ya Upanga, Posta, Tegeta, Mbagala, Tabata,
Kimara, Mbezi, Ukonga, Salasala, Mikocheni, Msasani, Sinza sasa watapata
huduma bora na upatikanaji wa intaneti ya kasi zaidi kupitia mtandao
wetu,"alisema Gutierrez.
Aliongeza
kuwa kampuni hiyo ipo mbioni kuzindua huduma ya 4G katika miji ya
Arusha , Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza na Tanga mwezi ujao na hivyo
kuifanya kampuni hiyo kuwa na mtandao mkubwa na wa kasi zaidi wa 4G
nchini.
Wakati
huohuo kampuni hiyo imeanzisha ushirikiano na kuunda mfuno wa utoaji
huduma za kimtandao usiotumia muindombinu asilia ya mawasiliano ambao
utaiwezesha UhuruOne kupanua upatikanaji wa teknolojia ya 4G na kwamba
mfumo huo ni wa kwanza barani Afrika.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab
Katunda alisema ''tunaiona Afrika ikichipua kiteknolojia lakini
kujumuisha uwanda mpana wa mawasiliano na dijitali kwenye uchumi wetu
kutautendea uchumi wetu jambo ambalo litatuneemesha sisi wenyewe na
kutuinua kimaisha".
0 comments:
Post a Comment