Leo
Watanzania watatumia haki yao ya kikatiba kuchagua Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Rais wa Zanzibar, wabunge wa Bunge la Muungano, madiwani na
wawakilishi kwa upande wa visiwani baada ya utawala wa Serikali ya Awamu
ya Nne kuhitimisha kipindi chake cha pili cha miaka mitano.
Ni
siku ambayo inahitimisha kampeni ya takriban siku 64 za wagombea wa
nafasi mbalimbali kujinadi kwa wananchi ili wapewe dhamana ya kuwaongoza
kwa miaka mitano ijayo.
Ni
siku ambayo Watanzania watakuwa wakipiga kura kwa mara ya tano kwenye
Uchaguzi Mkuu tangu mwaka 1995 baada ya Serikali kurejesha siasa za
ushindani mwaka 1992.
Katika uchaguzi wa mwaka huu, vyama nane vimesimamisha wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wagombea hao ni John Magufuli, anayegombea kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa (Chadema), Anna Mghwira (ACT Wazalendo) na Macmillan Lyimo wa TLP.
Wagombea hao ni John Magufuli, anayegombea kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa (Chadema), Anna Mghwira (ACT Wazalendo) na Macmillan Lyimo wa TLP.
Wengine ni Hashim Rungwe wa Chaumma, Chifu Litasola Yemba (ADC), Fahmi Dovutwa (UPDP) na Junken Kasambala wa NRA.
0 comments:
Post a Comment