Na: Hassan Hamad, OMKR.
Chama
Cha Wananchi CUF kimefunga rasmi kampeni zake za uchaguzi kwa upande wa
Zanzibar na kuwataka wadau wa uchaguzi kuheshimu maamuzi ya wananchi
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.
Akizungumza
kwenye mkutano huo wa ufungaji wa kampeni uliofanyika viwanja vya
Maisara Mjini Zanzibar, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema wananchi ndio wenye mamlaka ya
kuiweka Serikali madarakani, hivyo maamuzi watakayoyafanya kwenye
uchaguzi huo hayana budi kuheshimiwa.
Amerejea
kauli yake ya kukubali matokeo iwapo uchaguzi utafanyika kwa uwazi,
huru na haki na kuwashauri wagombea wengine wa Urais kutoa kauli kama
hiyo ili kuwaondoshea hofu wananchi.
Hata
hivyo amesema hatoridhia matokeo iwapo atashinda uchaguzi huo, na
kuelezea matumaini yake ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao.
Aidha
amesema atatumia uwezo wake kuviimarisha vikosi vya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na hana nia ya kumfukuza kiongozi yoyote wa vikosi
hivyo.
Amemshauri
Rais Kikwete na Dkt. Shein kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi ili
kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unafanyika katika hali ya Amani na
usalama.
Amesema
uchaguzi usiwe sababu ya kuvurugika kwa amani iliyopo na kuwataka
wananchi kushiriki kikamilifu kuhakikisha kuwa amani iliyopo inalindwa.
Amewataka
wananchi kuondosha hofu wanapokwenda kupiga kura na kumchagua kiongozi
wanayemtaka, na kwamba hakuna mwananchi atakayefuatiliwa au kujulikana
taarifa zake.
Nae
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chadema Mhe. Juma Duni Haji amesema ana imani kuwa Watanzania wako
tayari kwa mabadiliko.
Amesema
iwapo wananchi watawachagua wagombea wanaotokana na Umoja wa Ukawa
wataendeleza maridhiano na umoja wa wananchi, sambamba na kurejesha
katiba iliyopendekezwa na wananchi ambayo itato haki kwa wananchi wote.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Kampeni ya CUF Mansour Yussuf
Himid, amewataka wananchi kumchagua Maalim Seif ili aweze kuleta
mabadiliko ya kiuchumi nchini.
Amesema
Maalim Seif ni kiongozi anayejiamini, jasiri na mwenye uwezo wa
kuongoza nchi, na kwamba iwapo wazanzibari watafanya maamuzi sahihi
watajionea mabadiliko kwa kipindi kifupi baada ya uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment