Mgombea
Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, amepata
mapokezi makubwa mithili ya mfalme na wakazi wa jiji la Mbeya huku
baadhi ya wananchi walionekana wakifagia na kudeki barabara, wakati
akiwa njiani kuelekea eneo la Uwanja wa Rwanda Nzovwe, kulikofanyika
Mkutano wa hadhara wa Kampeni zake anazoendelea nazo kwa nchi nzima na
hii ikiwa hatua ya lala salama.
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa
UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,
Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", wakiwasili katika uwanja wa Rwanda Nzovwe
kwa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika Jijini Mbeya leo Oktoba
18, 2015.
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa
UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mbeya katika
Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda
Nzovwe, Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa
UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", wakati akizizungumzia
changamoto mbali mbali zinaziwakabili wananchi wa jiji hilo, katika
Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika Jijini Mbeya leo Oktoba 18,
2015.
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa
UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", wakati wa Mkutano wa
hadhara wa Kampeni, uliofanyika Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.
Waziri
Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Mji wa
Mbeya katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward
Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo
Oktoba 18, 2015.
Mwenyekiti
wa Chadema Taifa, Mh. Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa Jiji la
Mbeya waliofurika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wakati wa Mkutano wa
Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, leo Oktoba 18, 2015.
0 comments:
Post a Comment