Safari ya Marehemu Mchungaji Christopher Reuben Mtikila Duniani
imefika mwisho baada ya ndugu, jamaa, marafiki na mamia ya watu
kuongozana mpaka Kijiji cha Milo, Ludewa Mkoa wa Njombe ambapo
yamefanyika Mazishi yake jana October 08 2015.
Jina lake lilikuwa moja ya majina
makubwa sana kwenye Siasa kwa muda mrefu sana Tanzania, Msiba wake
umewashtua na kuwagusa watu wengi sana.
Marehemu Mchungaji Mtikila alikuwa
Kiongozi wa Chama cha Democratic Party (DP), na aliingia pia kwenye
Mchakato wa kugombea nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu Tanzania
October 2015, lakini kutokana na kutotimiza baadhi ya vigezo chama chake
kilitolewa na Tume ya Uchaguzi NEC katika kuendelea na mchakato huo.
Hizi hapa picha kutoka Kijiji cha Milo, Ludewa ambapo yamefanyika Mazishi ya Kiongozi huyo.
RIP Mchungaji Mtikila.
0 comments:
Post a Comment