STRAIKA wa Taifa Stars na TP Mazembe, Mbwana Samatta amesema
ana uhakika wataifunga Malawi, kesho Jumapili katika mchezo wa
marudiano na kutinga hatua ya pili ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la
Dunia 2018.
Samatta ambaye ni mfungaji wa bao moja
katika ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata Taifa Stars katika mchezo wa
kwanza jijini Dar es Salaam, aliliambia Championi Jumamosi kuwa,
mabadiliko makubwa wameyafanya hivyo ni lazima wavuke.
Akizungumza kabla ya kwenda Malawi, jana
Ijumaa, Samatta alisema: “Tunaondoka tukiwa na hamasa kubwa ya kupata
ushindi na kusonga mbele, kocha amerekebisha baadhi ya mambo aliyoyaona
awali.
“Kuna kitu tumekiweka sawa katika kiungo
na ushambuliaji kulingana na uchezaji wa Malawi na nina uhakika
tutafanya vizuri, Watanzania wasiwe na shaka, hatutawa-angusha.”
Kwa upande wake, straika mwingine wa
Taifa Stars anayechezea pia TP Mazembe, Thomas Ulimwengu alisema: “Tupo
vizuri kuhakikisha tunaifunga Malawi huku tukifahamu sisi ni msaada wa
timu.”
0 comments:
Post a Comment